Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wakulima pamba watakiwa kuongeza uzalishaji
Habari Mchanganyiko

Wakulima pamba watakiwa kuongeza uzalishaji

Spread the love

BODI ya Pamba Tanzania imewataka wakulima kuongeza uzalishaji kwa kanda ya Mashariki na kuondokana na umaskini kutokana na kupanda kwa bei ya Pamba hadi kufikia sh 1,560 ili kuwa na uwezo wa kuzalisha kama kanda ya Magharibi ambao huzalisha hadi asilimia 99 ya Pamba yote nchini. Anaripoti Christina Cosmas, Morogoro … (endelea).

Meneja wa huduma za usimamizi Bodi ya Pamba kanda ya Mashariki Emmanuel Mangulumba alisema hayo jana kwenye maonesho ya wakulima kanda ya Mashariki yanayofanyika kwenye viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere kuwa kilimo cha pamba hulimwa katika kanda mbili ambazo ni kanda ya magharibi yenye mikoa 12 na kanda ya mashariki ina mikoa mitano ambayo ina Iringa, Tanga, Morogoro, Kilimanjaro na Pwani.

Alisema mpaka sasa uzalishaji kitaifa ni asilimia 99 na hutoka kanda ya Magharibi na Mashariki huzalisha asilimia moja hadi chini ya asilimia moja lakini azimio la Serikali ni kuwatoa kwenye umakini wananchi  kupitia kilimo cha Pamba ambapo zao la Pamba lilianzia Kanda ya Mashariki ambako maisha ya watu yalikuwa mazuri na kwamba kupitia zao hilo Serikali imeona kuwa wananchi wanaweza kutoka kwenye umaskini.

Alisema msimu uliopita 2021 walizalisha kilo laki 314 lakini kwa msimu huu 2022 wanategemea kuzalisha mara 10 zaidi ya hiyo kutokana na jitihada zinazofanyika kupitia wadau ikiwemo bodi ya Pamba wenyewe na Mwekezaji Upami Agrobussiness ambao wanahamasisha pamba kwa wakulima katika eneo lote la kanda ya Mashariki.

Mangulumba alisema kwa upande kama bei itakuwa hiyo na kuendelea kupanda wanategemea ifikapo mwaka 2025 mpaka 2030 waweze kuzalisha angalau zaidi ya kilo mil 10 kwa kanda ya mashariki.

Alisema wanaendelea na jitihada za kuwasaidia wakulima wa Pamba kwa mbegu, mbolea na pembejeo kwa mkopo ili kilimo hicho kiweze kuboreshwa kwenye kanda ya mashariki.

Naye Mkurugenzi wa kampuni ya uwekezaji wa Pamba Kanda ya Mashariki Upami AgroBusiness Ltd Vitus Lipagila alisema anajipanga kuhakikisha pamba inalimwa zaidi kanda ya mashariki kwa sasa na kuondoa changamoto ya wakulima kukosa soko baada ya kuwepo wanunuzi wanaotoka kanda ya magharibi pekee.

Lipagila alisema tayari kampuni yake imeshafufua viwanda viwili vya kuchakata Pamba ambavyo vipo katika wilaya za Kiku – Kilosa na Koreko cha mkoa wa Pwani ambavyo tayari ameshaingia navyo mkataba na vinafanya kazi na kwamba anatarajia kujenga kiwanda kikubwa maeneo ya Lupilo- Mahenge wilayani Ulanga mkoani hapa.

Alisema kwa msimu wa kilimo wa mwaka huu kanda ya Mashariki wanatarajia kuvuna kilo mil 2 na kidogo ambazo ni mwanzo mzuri sababu ni kitu ambacho hawakutegemea kabisa.

Aliwataka wakulima kuondoa hofu ya kuuza kwa mkopo bali kwa sasa wao Upami wananunua kwa pesa taslimu na kufanya wakulima kuendelea kunufaika na zao hilo katika kutatua changamoto zao za kifamilia kwenye maisha yao ya kila siku.

Naye Afisa Kilimo zao la Pamba kanda ya Mashariki Alphonce Ngawagala aliwataka wakulima kuzingatia vipimo vya upandaji Pamba katika mashamba ambayo hayatuamishi maji ili kupata uzalishaji wa kutosha.

Ngawagala alisema kabla hawajaanza hamasa tayari wakulima wameshaanza kuongeza kulima ambapo kwa msimu watakaoenda wa kilimo mwaka 2023 tayari wakulima wameshaonesha nia ya kuongeza Mashamba na wanahitaji pembejeo mbegu.

Alisema msimu huu wa kilimo pamba ipo shambani inavunwa na wengine wameshaanza kuuza  ambapo wakulima wana jumla ya hekari 9,579 ambapo awali walikuwa na hekari 3000.

Aidha alisema kwa sasa inajionesha kuwa wakulima wameshaona zao hilo linawaokoa kiuchumi sababu ya kuwa na uhakika wa soko na kupanda kwa bei ya mauzo kwa kila mwaka.

Hivyo aliwaasa wakulima kurudi kwenye zao la pamba kwa sababu changamoto zilizokuwepo siku za nyuma zimeshatatuliwa ikiwemo masoko.

Naye mmoja wa wakulima wa Pamba Arold Mteme alishukuru Bodi ya Pamba kwa kuongeza bei na kiwawekea wakala Kanda ya Mashariki atakayenunua na kuwalipa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

Habari Mchanganyiko

Jeshi la Uhifadhi kujengewa uwezo zaidi

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imejipanga vyema kuendelea kulijengea...

Habari Mchanganyiko

Wanavyuo Dodoma waonja utamu wa chimbo la nyuki

Spread the love  TAMASHA la Chimbo la Nyuki lililofanyika katika Ukumbi wa...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

Wakili Mwabukusi anusurika kufungiwa, asema hatarudi nyuma

Spread the loveWAKILI Boniface Mwabukusi amesema kuwa hatorudi nyuma kuwatetea Watanzania na...

error: Content is protected !!