Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko Barabara ya Kimara – Kibaha njia nane kukamilika Oktoba
Habari Mchanganyiko

Barabara ya Kimara – Kibaha njia nane kukamilika Oktoba

Spread the love

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya amemtaka Mkandarasi anayejenga Barabara ya Kimara – Kibaha (Km 19.2), pamoja na Barabara za maingilio katika Kituo Kikuu cha Mabasi yaendayo mikoani Mbezi-Magufuli kuhakikisha ujenzi huo unakamilika ifikapo Oktoba mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na wanahabari jana tarehe 10 Agosti baada ya kukagua barabara hiyo jijini Dar es Salaam, Mhandisi Kasekenya amesema Serikali imeridhishwa na uboreshaji wa barabara za maingilio na madaraja katika eneo la mbezi hivyo kumtaka mkandarasi kumaliza kazi hiyo haraka iwezekanavyo na kwa ubora.

Amebainisha kuwa katika mkakati wa kupunguza msongamano jijini Dar es salaam tayari maandalizi ya kujenga kwa njia nane sehemu ya Kimara hadi Ubungo yameanza ili kuhakikisha hakuna msongamano wa magari kati ya  Ubungo-Kibaha.

“..Asilimia 88 iliyofikia inatosha kukamilisha kazi zilizobaki katika kipindi cha miezi miwili ijayo, hivyo TANROADS na Mkandarasi ESTIM hakikisheni kazi hiyo inakamilika kwa ubora,” alisisitiza.

Aidha amewaonya wezi wa miundombinu ya taa za barabara kuacha kufanya hivyo mara moja kwani usalama wa barabara ni pamoja na uwepo wa taa hizo, na kusisitiza umuhimu wa wananchi kutumia madaraja ya juu na kuvuka katika maeneo yaliyotengwa ili kupunguza ajali.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Mhandisi Godfrey Kasekenya akisisitiza jambo kwa wataalam wanaosimamia ujenzi wa Barabara ya Kimara – Kibaha (Km 19.2), ambao ujenzi wake unaendelea jijini Dar es Salaam.

Naye Mhandisi Mkazi anayesimamia ujenzi wa Barabara hiyo, Mwanaisha Rajabu amemhakikishia Naibu Waziri Kasekenya kuwa atahakikisha barabara hiyo inakamilika kwa wakati na ubora uliokusudiwa ifikapo Oktoba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Puma Energy Tz: Watanzania tudumishe amani kuvutia uwekezaji

Spread the loveKAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha wadau mbalimbali katika...

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

error: Content is protected !!