Monday , 5 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Wahalifu 284 watiwa nguvuni Dar
Habari Mchanganyiko

Wahalifu 284 watiwa nguvuni Dar

Lucas Mkondya, Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam
Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limefanikiwa kukamata jumla ya wahalifu 284 katika operesheni iliyochukua siku 20, anaandika Yasinta Francis.

Katika operesheni hiyo iliyoanza tarehe 28 Mei, 2017 mpaka 18 Juni, 2017 polisi walifanikiwa kuwakamata wahalifu 284 wanaotuhumiwa kufanya makosa mbalimbali ikiwemo, utapeli, ujambazi na matumizi ya dawa za kulevya.

Lucas Mkondya, Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amesema operesheni hiyo ni endelevu na inalenga kudhibiti vitendo vya uhalifu ndani ya jiji la Dar, na kwamba wananchi watoe ushirikiano katika kufichua wahalifu wanaoishi katika makazi yao.

Miongoni mwa wahalifu waliotiwa nguvu na polisi ni Abdillah Rashid mkazi wa Mbande ambaye amekamatwa akiwa na risasi 117 za SMG/SR zikiwa kwenye mfuko wa kaki.

”Huyu tulimkamata tarehe 8 Juni, mwaka huu ambapo askari wakiwa katika doria walimkamata Abdillah Rashid mkazi wa Mbande akiwa na risasi 117 za SMG/SR zikiwa kwenye mfuko hata hivyo mtuhumiwa huyo anaendelea kuhojiwa na atafikishwa mahakamani, uchunguzi utakapokamilika,” amesema Kamanda Mkondya.

Aidha polisi pia walimkamata Idd Ally mkazi wa Kijichi akiwa na silaha bandia “pistol toy” ambapo baada ya kuhojiwa alikiri kuwa amekuwa akitumia katika matukio mbalimbali ya kuwatishia watu na kisha kuwapora.

“Tunaendelea kudhibiti wahalifu na tunatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za uhalifu pindi zinapotokea kwa kupiga simu namba 0787 668 306 ambayo utapata msaada kwa haraka,” amesema.

Mbali na kukamata wahalifu lakini pia jeshi la polisi limefanikiwa kukamata jumla ya kete 94 za dawa za kulevya, vifaa vya kuandalia bangi 119, misokoto ya bangi 112 na pombe haramu ya gongo lita 103.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

Habari Mchanganyiko

Bandari ya Kigoma kuongezewa uwezo wa kutoa huduma zake

Spread the love  SERIKALI kupitia mamlaka ya Bandari nchini (TPA), imewekeza takribani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kifo cha mwanafunzi UDOM: Tume yamsafisha naibu waziri

Spread the loveTUME ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini (THBUB),...

error: Content is protected !!