Tuesday , 27 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi Dar: Kipigo kwa walemavu kilikuwa halali
Habari Mchanganyiko

Polisi Dar: Kipigo kwa walemavu kilikuwa halali

Lucas Mkondya, Kaimu Kamishna wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam
Spread the love

SIKU tatu baada Jeshi la Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuonekana wakiwaadhibu watu wenye ulemavu waliokuwa wakifanya maandamano kupinga kuzuiwa kuingia katikati ya jiji, polisi wamesema, ulemavu si kibali cha kuvunja sheria, anaandika  Yasinta Francis.

Lucas Mkondya, Kamanda  wa  Polisi  Kanda  Maalum Dar es Salaam amesema nguvu iliyotumiwa na polisi haikuwa kubwa na kwamba walemavu hao walifunga njia na kuvamia ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Ilala na walikaidi maagizo ya jeshi hilo.

“Ulemavu si kibali cha kuvunja sheria. Hawa walemavu walifanya makosa, walivamia ofisi ya manispaa, wakafunga njia na tulipowasihi wafungue njia na wateue viongozi wa kushughulikia matatizo yao walikaidi.

“Ikabidi tutumie nguvu kidogo tu kwenda kuwaondosha. Walemavu wajaribu kuheshimu sheria za nchi kwani sheria za nchi ni lazima zisimamiwe. Polisi tukiona sheria zinavunjwa lazima tusimamie, ambaye hataki kukumbana na mkono wa polisi basi atii sheria za nchi,” amesema Kamanda Mkondya.

Amekanusha taarifa kuwa nguvu iliyotumika kuwadhibiti walemavu hao ilikuwa ni kubwa kupitiliza, pamoja na madai ya kuwepo kwa uvunjifu wa haki za binadamu.

Tukio la kukamatwa na kupigwa kwa walemavu lilitokea tarehe 16 Juni, 2017. Pamoja na mambo mengine lakini walemavu hao walikuwa wakipinga agizo la serikali la kuwataka walemavu kutoingia katikati ya jiji wakiwa na pikipiki za miguu mitatu na  kuegesha  katikati  ya jiji.

Madai  hayo  ya  walemavu  yanalindwa  na  Mkataba  wa  Kimataifa  wa Haki za watu wenye Ulemavu Ibara  ya 9 wa mwaka 2006.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mafua yamtesa Papa, afuta mikutano

Spread the loveKiongozi wa Kanisa katoliki duniani, Papa Francis amelazimika kufuta mkutano...

Habari Mchanganyiko

Oryx wagawa mitungi 1000 kwa viongozi wa dini, wajasiriamali Moshi

Spread the loveVIONGOZI wa dini kutoka madhehebu mbalimbali pamoja na wajasiriamali katika...

Habari Mchanganyiko

RC Geita awafunda wahitimu wapya GGML

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela ametoa wito kwa...

Habari Mchanganyiko

Biteko asisitiza umuhimu wa EREA sekta ya nishati

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!