August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mafia walia na vifaa tiba vya watoto njiti

Spread the love

UONGOZI wa hospitali ya Mafia, iliyopo mkoa wa Pwani umeiomba serikali na wadau wa maendeleo kusaidia upatikanaji wa vifaa tiba kwa ajili ya kuwahudumia watoto njiti wanaofariki kwa kukosa huduma zitokanazo na vifaa hivyo, anaandika Shafiyu Kyagulani.

Abdallah Bahi, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mafia amesema tatizo la vifaa tiba vya kuhudumia vifaa tiba limekuwa likisababisha watoto wengi kufariki baada ya kuzaliwa.

“Serikali na watu wengine wenye uwezo, wajitokeze kutusaidia vifaa tiba vya kuwahudumia watoto wanaozaliwa kabla ya umri wao, kwa kuwa watoto wengi wanafariki kwa kukosa huduma za msingi,” amesema.

Ameeleza kuwa kwa mwezi mmoja huzaliwa wastani wa watoto nane hadi kumi katika hospitali hiyo, hali inayowapa shida kuwahudumia kutokana na kukosa vifaa kama vifaa kwa ajili ya kuwasaidia kupumua, na mashine za kusaidia kunyonya uchafu.

“Watoto wengi wapoteza maisha kutokana na kukosa vifaa tiba, lakini pili ni umbali uliopo na gharama za usafiri maana Mafia ni kisiwa na usafiri wetu ni mpaka ndege na boti ndogo ambazo pia hazina uwezo mkubwa,” amesema Abdallah Bahi.

error: Content is protected !!