Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe limewakamata watuhumiwa 11 kwa kufanya shughuli za uganga bila kuwa na kibali. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Taarifa iliyotolewa na leo Alhamis Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe, Thoepista Mallya imesema watuhumiwa hao wakamatwa kutokana na operesheni iliyofanywa na jeshi hilo tarehe 9 Januari mwaka huu.
Amewataha watuhumiwa hao kuwa ni Chifu wa kabila la Kinyiha aitwaye Mwene Nzunda (44) mkazi wa kiji cha Nambala pamoja na wenzake ambao ni Anthony Yatilinga Mapumba (G5) mkazi wa llembo, Isambi Yasinta Mghallah (80) mkazi wa Majengo, Kostebo Ngawelo Mziho (53) mkazi wa Nambala.
Wengine ni Tamimu Balison Mdolo (57) mkazi wa lembo, Biton Daimon Nzunda (64) Balozi mtaa wa Nsenya Shina namba 8 na mkazi wa Nsenya, Amnos Nzunda (23) Steven Mwilenga (46) David Frank Mapumba (72) mkazi wa llembo, George Greyson Mghala (43) mkulima, mkazi wa mtaa wa Danida katika kijiji cha llembo na Jailos Sola (42) mkulima na mkazi wa Mbimba.
Kwa melezo ya watuhumiwa hao wanasema kwamba katika kiji hicho kuna mambo yanayofanyika yanayoashiria kuwa ni yakishirikina.
Aidha amesema Jeshi la Polisi linakamilisha upelelezi wa kesi hi ili watuhumiwa waweze kufikishwa mahakamani.
“Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Songwe kuwa ni marufuku kwa mtu yoyote kufanya shughuli za uganga bila kibali ikiwa ni pamoja na kitendo cha kusafisha nyumba zinazodhaniwa kuwa na uchawi kwani kitendo hicho kinaleta chuki na udhalilishaji kwa jami.
“Pia kwa mtu yoyote anapotaka kufanya kusanyiko lolote ni lazima viongozi wa sehemu husika wajulishwe,” amesema.
Leave a comment