Friday , 17 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Wananchi wafurahishwa na elimu ya Hali ya Hewa Zanzibar
Habari Mchanganyiko

Wananchi wafurahishwa na elimu ya Hali ya Hewa Zanzibar

Spread the love

 

WANANCHI kutoka maeneo mbalimbali Zanzibar, wamefurahishwa na elimu ya hali ya hewa inayotolewa katika maonesho ya Maadhimisho ya miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, yanayofanyika katika viwanja vya Maonesho ya Biashara, Nyamanzi, Mjini Magharibi, Zanzibar kuanzia Tarehe 07 – 19 Januari, 2024. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar … (endelea).

Wageni mbalimbali waliweza kutembelea banda la TMA wakiwemo viongozi wa Taasis kutoka Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) Prof. Ulingeta Mbamba, Shirika la Reli Tanzania  Masanja Kadogosa, Mkurugenzi wa Huduma za Taasis kutoka Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), Hamidu Mbegu, Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) Teophoy Mbilinyi ambao waliipongeza TMA kwa huduma nzuri ya usahihi wa Utabiri inayotolewa.


Aidha, wataalam wa hali ya hewa kutoka TMA wameendelea kutoa elimu kwa wadau mbalimbali ili kutumia huduma mahususi zinazotolewa na TMA pamoja na kuelewa namna ya kutumia taarifa za hali ya hewa kwa usahihi ili kukabiliana na athari zitokanazo na hali mbaya ya hewa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara yaomba bajeti ya Sh. 67.9 bilioni, wamachinga watengewa bilioni 10

Spread the loveBAJETI ya Wizara ya maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na...

Habari MchanganyikoTangulizi

Migogoro ya ndoa yaongezeka, Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveMIGOGORO ya ndoa na familia imeongezeka kwa asilimia 8.3  kutoka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yahamasisha uanzishaji vituo vya kulea watoto wachanga

Spread the loveSERIKALI imewahimiza wananchi kujenga vituo vya kulelea watoto wadogo na...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Udhibiti wa serikali wakera asasi za kiraia

Spread the loveBaadhi ya wadau wa demokrasia na viongozi wa asasi za...

error: Content is protected !!