Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wadau mbegu asili watakiwa kujikita kwenye tafiti
Habari Mchanganyiko

Wadau mbegu asili watakiwa kujikita kwenye tafiti

Mwenyekiti wa Shirika la Kuendeleza Kilimo Hai Tanzania (TOAM), Dk Mwatima Juma akizungumza na wadau wa mbegu asili jijini Dodoma.
Spread the love

MWENYEKITI wa Shirika la Kuendeleza Kilimo Hai Tanzania (TOAM), Dk. Mwatima Juma amewataka wadau wa mbegu asili na zilizosahulika kujikita kwenye utafiti, ili kushawishi mamlaka kwanini wanataka mbegu hizo kupewa kipaumbele. Anaripoti Selemani Msuya… (endelea).

Dk. Mwatima ametoa rai hiyo jana tarehe 9 Novemba, 2022 wakati akizungumza na wadau hao waliokutana kwa siku tatu jijini Dodoma katika kongamano la kujadili hatma ya mbegu asili na zilizosahaulika hapa nchini na duniani kwa ujumla.

Ofisa Mperembaji wa Shirika la Kuendeleza Kilimo Hai Tanzania (TOAM), Paul Chilewa akifafanua jambo kwenye mkutano wa wadau wa mbegu asili

Mkutano huu umeshirikisha wadau kutoka Shirika la SWISSAID Tanzania, Alliance for Food Sovereignty in Afrika (AFSA), TOAM, Shirika la Kuendeleza Kilimo Hai Barani Afrika (AFRONET), PELUM Tanzania, Mkulima Mbunifu, Shirika la Kilimo Endelevu Tanzania (SAT), ECHO East Afrika na wengine.

Mwenyekiti huyo alisema kuzungumza na kuhamasisha kilimo hai cha kutumia mbegu asili kila siku, kunaweza kuwa na matokeo chanya iwapo kutakuwa na taarifa za kitafiti.

“Hawa wafanya maamuzi wana mambo mengi, jambo la kusisitiza na kuwabana ni sisi wadau wa mbegu asili kuonesha ushahidi wa kitafiti za kisayansi ambazo zitaweza kuwashawishi kuweka mkazo katika eneo hilo,” alisema.

Dk. Mwatima alisema kila taasisi ambayo inahamasisha matumizi ya mbegu asili inapaswa kutenga fedha kwa ajili ya utafiti, pamoja na kutoa elimu kwa wakulima umuhimu wa mbegu hizo.

Alisema pamoja na utafiti ambao unatakiwa kufanyika ni vema kuonesha athari ambazo ardhi imepata kupitia kilimo ambacho hakitegemei mbegu asili.

Mwenyekiti huyo alisema iwapo kundi hilo la mbegu asili litakuwa na misimamo ya pamoja katika kupigania kilimo hai cha kutumia mbegu asili ni wazi kuwa ajenda hiyo itaweza kunusuru jamii na taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyingine, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la Kuendeleza Kilimohai Barani Afrika (AfrONet) Constantine Akitanda, amekieleza kikao cha wadau wa mbegu mjini hapa kuwa bara la Afrika lina kila sababu ya kuzalisha chakula cha kutosheleza mahitaji ya watu wake wote.

“Ni lazima nchi ijielekeze katika kuongeza uzalishaji wa mazao yaliyotelekezwa ama mazao yatima, mazao haya yana nutrisheni ya kutosha na ni miongoni mwa mazao yanayohimili ukame, yanastawi hata katika ardhi isiyo na rutuba ya kutosha na kuhimili magonjwa” alisema.

Akitanda alisema kufuatia mabadiliko ya tabianchi kuendelea kuiathiri dunia, uzalishaji wa mazao yaliyozoeleka kama mahindi, mpunga na ngano ambao kwa sehemu kubwa unategemea mvua, ni wazi kwamba mahitaji ya kujitathimini ni makubwa zaidi ili kuwa na mkatati thabiti wa kupanua wigo wa mazao yatima.

Tanzania kama zilivyo nchi nyingine za Kiafrika lazima iwe mstari wa mbele ili isiachwe nyuma katika kujihakikishia usalama wa chakula siku za mbeleni.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!