Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wadau haki binadamu wataka mfumo wa jinai ufumuliwe
Habari Mchanganyiko

Wadau haki binadamu wataka mfumo wa jinai ufumuliwe

Fatuma Karume, aliyekuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS)
Spread the love

WADAU wa masuala ya utetezi wa haki za binadamu, wameshauri mfumo mzima wa haki jinai nchini ufumuliwe kwa maelezo kwamba haukidhi mahitaji ya sasa kwa kuwa ulianzishwa kwa misingi ya kikoloni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Ushauri huo umetolewa Leo tarehe 11 Machi 2023, katika kongamano la wazi la kukusanya malni ya wadau juu ya namna ya kuboresha mfumo wa haki jinai nchini, lililoandaliwa na Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), na kufanyika jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya taasisi za mfumo huo zilizotajwa kuwa na mapungu ni, Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Mahakama na Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP).

Aliyekuwa Rais wa Chama Cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Fatma Karume, ameshauri Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka iboreshwe ili kuhakikisha haki jinai inapatikana kwa mujibu WA Sheria.

Fatma amesema kuwa, ofisi hiyo inakabiliwa na changamoto ya kunyuma dhamana mahabusu wanaokabiliwa na mashtaka mbalimbali mahakamani, kitendo kinachoepelekea mrundikano wao gerezani.

Wakili mwandamizi, Mpare Mpoki, amesema mfumo mzima wa haki kijana umekufa hivyo unapaswa kufufuliwa ili kuboresha upatikanaji wa haki hiyo.

Ametaja baadhi ya taasisi za haki jinai zinazopaswa kuboreshwa ikiwemo Jeshi la Polisi, ambapo ameshauri libadilishwe ili lisiwe jeshi badala yake iwe taasisi ya kutoa huduma. Huku akitaka magereza iwe shule ya kurekebisha badala ya gereza la kuadhibu watu.

Aidha, Wakili Mpoki ameshauri sheria ziweke wazi taasisi zenye wajibu wa kutoa elimu ya haki jinai kwa wananchi.

Naye aliyekuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Beatus Malima, ameshauri vyombo vinavyotoa haki jinai hususan Jeshi la Polisi, viboreshwe ili kuondoa changamoto ya kesi za kubambikizwa na watu kukamatwa kinyume cha sheria.

“Mfano mtu amekamatwa lakini waliomkamata wanakataa kutoka taarifa keamba tumemkamata tunaye mahali fulani, wananchi wanapiga kelele zikiwa ndogo inaisha lakini zikiwa kubwa mwishowe wanajitokeza watu wanasema tunaye, hali hi inajitokeza kwa sababu ya kesi za kubambikiza wanawakuwa hawana ushahidi na wanataka wamtumie wanavyotaka,” amesema Malima.

Naye Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TWLA), Tike Mwambikile, ameshauri Jeshi la Magereza liboreshwe ili kulinda haki za mahabusu na wafungwa.

Amedai kwa sasa mahabusu wanachanganywa sehemu moja na wafungwa hususan waliohukumiwa kwa makosa makubwa, kitendo kinachowaathiri kisaikolojia ilhali mahakama haijaamua kama wana hatia au lah!

Aidha, ameshauri mahakama za watoto wanaokinzana na sheria ziboreshwe ili ziweze kutoa elimu kwa watoto hao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!