Thursday , 18 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia ampandisha cheo RPC wa Dar
Habari MchanganyikoTangulizi

Rais Samia ampandisha cheo RPC wa Dar

Spread the love

MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Camillus Wambura, amesema Rais Samia Suluhu Hassan, amempandisha cheo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar ea Salaam (RPC), Jumanne Muliro kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizj wa Polisi (SACP). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania, SACP David Misime, uteuzi wa Kamanda Muliro, aliyekuwa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), amepandishwa cheo kuanzia tarehe 20 Februari 2022.

“Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Camillus M.Wambura anapenda kuwajulisha kuwa Dk. Samia Suluhu Hassan ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama,” imesema taarifa hiyo na kuongeza:

“Amempandisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Muliro Jumanne Muliro kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP).

Amepandishwa cheo hicho kuanzia tarehe 20 Februari 2023.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

Habari Mchanganyiko

Serikali yatoa ajira watumishi 46,000, yatangaza utaratibu mpya kuajiri

Spread the loveSERIKALI imetangaza nafasi za ajira za watumishi wa umma 46,000...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia kutunukiwa udaktari wa heshima Uturuki

Spread the loveBaraza la Chuo Kikuu cha Ankara, ambacho ni cha pili...

Habari za SiasaTangulizi

Rais Samia atua Uturuki kwa ziara ya siku 5

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan leo Jumatano amewasili nchini Uturuki kwa...

error: Content is protected !!