Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Wachimbaji wadogo waitwa maonesho madini Geita, kampuni 600 zashiriki
Habari Mchanganyiko

Wachimbaji wadogo waitwa maonesho madini Geita, kampuni 600 zashiriki

Spread the love

KATIBU Mkuu Wizara ya Madini, Adolf Ndunguru ametoa wito kwa wachimbaji wadogo wa madini nchini kushiriki Maonesho ya 5 ya Teknolojia ya Madini 2022 mkoani Geita kwa lengo la kujifunza namna bora ya utendaji wa shughuli zao. Anaripoti Paul Kayanda, Geita.. (endelea).

Ndunguru ametoa kauli hiyo jana tarehe 27 Septemba, 2022 alipotembelea mabanda ya maonesho hayo yaliyoanza mkoani Geita.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo akizungumza na waandishi wa habari

Amesema wizara ya madini inayo mikakati mbalimbali ya kuwasaidia wachimbaji wadogo ili wapate elimu ya uchimbaji madini na hatimaye waweze kuchimba kwa tija

Aidha, amesema Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) pamoja na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) wapo kwenye maonesho hayo kwa lengo la kuwasaidia wachimbaji wadogo ili kupata taarifa sahihi ya uwepo wa madini katika maeneo yenye uchimbaji.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Msafiri Mbibo amewapongeza waandaaji wa maonesho hayo na kuwataka kuzibainisha changamoto zilizojitokeza kwa lengo la kuboresha zaidi katika maenesho yatakayofuata ya mwaka 2023.

“Nimepata taarifa kwamba, zaidi ya kampuni na taasisi 800 zimealikwa kushiriki katika maonesho haya lakini kampuni 602 ndiyo zimethibitisha kushiriki hivyo, niuombe mkoa wa Geita na waandaaji wote kwa ujumla kuendelea kuyatangaza maonesho haya ili wadau wa madini wa ndani na nje ya nchi washiriki kwa wingi zaidi,” amesema Mbibo.

Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Adolf Ndunguru akizungumza na waandishi wa habari.

Pia, Mbibo amesema maonesho hayo yanalenga kutangaza fursa za uwekezaji zilizopo kwenye Sekta ya Madini kwa lengo la kuvutia wawekezaji ili kuchochea uchumi wa Taifa.

Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu Ndunguru ameambatana na Naibu Katibu Mkuu Mbibo, Kamishna wa Madini Dk. Abdulrahman Mwanga na Mtendaji Mkuu wa GST Dk. Mussa Budeba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!