SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limewataka waagizaji wa magari yaliyotumika kutoka Japan, mawakala wa forodha na wananchi wote kwa ujumla kuhakikisha wanakagua magari hayo kabla ya kusafirishwa kuja Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Taarifa iliyotolewa leo tarehe 28 Septemba, 2022 na Meneja Uhusiano na Masoko kutoka TBS, Gladness Kaseka imesema watakaoshindwa kukidhi matakwa hayo watakumbana na adhabu.
Imesema Shirika litalazimika kuyakagua magari hayo hapa nchini sambamba na adhabu ya asilimia 30 ya jumla ya gharama ya gari husika na usafiri (Cost and Freight) kwa kuzingatia nyaraka za kodi zilizohakikiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Hayo yanajiri baada ya Shirika hilo kutoa taarifa tarehe 20 Julai, 2022 kwamba magari yote yaliyotumika (used motor vehicles) yanayotoka nchini Japan yatakuwa yanakaguliwa nchini Japan kabla ya kuja Tanzania kwa utaratibu wa Pre-Shipment Verification of Conformity to Standard (PVoC).
Leave a comment