Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge waijia juu Toyota Tanzania, Spika aomba majibu
Habari za Siasa

Wabunge waijia juu Toyota Tanzania, Spika aomba majibu

Gari aina ya Toyota Land cruiser V8
Spread the love

 

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Dk. Tulia Akson, ameitaka Serikali kutoa majibu hoja ya suala la Serikali kushindwa kuagiza magari moja kwa moja kutoka kwa mzalishaji na badala yake kutumia wakala. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Dk. Tulia amesema hoja hiyo inafanana na suala la uagizaji wa mafuta ambayo mara nyingi hutumia mawakala badala ya kwenda kwa wazalishaji moja kwa moja.

Spika ameyasema hayo leo Alhamisi tarehe 23 Juni, 2022 baada ya Mbunge wa Viti Maalum, Riziki Lulida kuhoji sababu ya Toyota Tanzania kumiliki soko na kusababisha watanzania kushindwa kununua magari mapya kiwandani.

“Kama ndivyo Waziri atakuja kutuambia, najua huwezi kujibu hoja zote lakini hili tungependa kuisikia kwamba watu hawawezi kuagiza magari zero mileage bila kupitia Toyota litakuwa jambo la ajabu sana,” amesema.

Spika amesema jambo hili linafanana na lile la mafuta kwamba huwezi kwenda moja kwa moja kwa wazalishaji, “sasa kama inawezekana ni vizuri watanzania wajue ili wachangamkie fursa hiyo.”

Awali akichangia hoja hiyo Lulida amesema wakala wanauza magari wameingia makubaliano na wazalishaji nchini Japan ya kuzuia mtu kununua gari jipya moja kwa moja hadi apitie kwao.

Ameongeza kuwa gharama ya kununua gari Tanzania ni mara mbili ya bei wanayonunua Kenya na Uganda.

“Tumefika wapi tujitambue, kwanini tunaendelea kuchezewa namna hii,” amesema na kuongeza kuwa yeye ni mwathirika wa kununua magari mapya ya Toyota kwa bei mara mbili ya ile inayouzwa Kenya.
“Nataka Waziri ajibu hoja hii.”

Amesema UNDP ni taasisi inayoleta magari taznaia kwaajili ya miradi yao lakini hata wao wamezuiwa kununua gari jipya kutoka kwa wazalishaji na kutaka Sheria ya Manunuzi ya mwaka 2013 kubadilishwa kwani “ni mwiiba kwa nchini hii”.

“Haikubaliki tunaangaika kutafuta fedha kutoka kwa wananchi masikini halafu mwisho mtu mmoja anachukua donge lote anakaa nalo pembeni, tusikubali muda wa kutufanya shamba la bibi limepitwa na wakati watanzania sasa tumefunguka tunataka maonevu yote yanashughulikiwa,” amesema.

Mbali na Lulida Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku, ametoa mfano wa yeye mwenyewe kununua gari mara mbili ya bei za kawaida.

“Leo ukitaka kuagiza Toyota mpya kama hili la Waziri wa Fedha inauzwa dola 140,000 pamoja na ushuru lakini mimi nikiiagiza hiyo gari ushuru wake tu ni Sh210 milioni halafu kununua dola 140,000, yaani ushuru umewekwa mara mbili ili ulazimike kupitia Toyota,” amesema.

Naye mbunge wa Manyoni Magharibu, Yahaya Massare, amesema Toyota Tanzania ni wakala wa mzalishaji aliyepo Japan hivyo amemiliki soko “kiasi kwamba wewe huweza kwenda kule kwenye soko.”

Amesema hoja ya Lulida ni kwamba “kuna uvivu tu wa watu wetu wamekubali kuingia kwenye mtego wa Toyota Tanzania ambaye ni agent wa mtengenezaji kwanini serikali isiagize kiwandani moja kwa moja?”

1 Comment

  • Loh!
    Nyie wabunge si milipitisha sheria ya manunuzi.
    Nyie wabunge si mlipitisha “Sheria ya Ushindani”
    Nyie wabunge si mliipa “Tume ya Ushindani” rungu koko.
    Nyie wabunge si mna mazoea ya kufanya sheria za umma siri bila kuchapisha vitabu vya sheria watu wanunue na kuzisoma.
    Nyie wabunge si mmewapa hao watu uwezo wa kuendesha 60% ya uchumi wetu.
    Nyie wabunge si ndio mliokosa uzalendo!
    Sasa mnalalamika badala ya kusafisha hizi sheria. Hayo maneno yayavunji mfupa!
    Mtakeni Waziri au muiitishe na kurekebisha.
    Acheni kulalamika sasa. Chapeni kazi ya kurekebisha sheria hiyo.
    Msipoirekebisha, basi mmehongeka na wananchi wanateseka kununua magari mitumba. Si lazima kuwe na ushahidi, bali kuna tabia ya kuruhusu MONOPOLY iliyo kinyume na COMPETITION.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!