Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Serikali yashauriwa namna ya kushawishi wananchi kuhama Ngorongoro
Habari Mchanganyiko

Serikali yashauriwa namna ya kushawishi wananchi kuhama Ngorongoro

Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania imeshauriwa kutumia njia shirikishi katika utatuzi wa mgogoro wa ardhi kwenye Hifadhi ya Ngorongoro, mkoani Arusha, ili wananchi watoe ushirikiano katika zoezi la uwekaji mipaka ya ardhi na kuhama kwa hiari kuelekea Kijiji cha Msomera, wilayani Handeni mkoani Tanga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, leo Ijumaa, Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Onesmo Olengurumwa, amesema mazoezi hayo yanakabiliwa na ukinzani kutoka kwa wananchi kutokana na Serikali kutowashirikisha kikamilifu.

Olengurumwa amesema, nia ya Serikali kuwahamisha wananchi kwenda Msomera kwa ajili ya kupunguza changamoto ya ongezeko la idadi ya watu, makazi na mifugo hifadhini hapo, ni njema lakini inakwama kutokana na wananchi kutopewa nafasi inavyostahili.

“Serikali itumie njia shirikishi kwa kuhakikisha huduma za kijamii zinakuwepo kwa wanaobaki sababu wanakabiliwa na changamoto ya kuishi katika mazingira magumu inabidi nao wapewe haki. Wanaobaki wasionekane wamefanya kosa kubaki pale na wanaoondoka kwa hiari wapewe haki zao huko wanakokwenda,” amesema Olengurumwa.

Olengurumwa amesema kuwa, wananchi wa Ngorongoro walipaswa kupewa tuzo kwa kuhifadhi eneo hilo, badala ya kuandikwa vibaya katika baadhi ya vyombo vya habari.

Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa

“Kilichokwamisha zoezi la uwekaji alama za mipaka na wananchi kuhama kwa hiari ni ile njia ya kuwaandika vibaya kwenye magazeti. Nadhani wangewapa hata tuzo kwa kutunza eneo la Loliondo. Lakini kupelekwa vikosi ni njia mbaya,” amesema Olengurumwa na kuongeza:

“Wananchi walikuwa tayari kushirikiana na walikubali eneo libaki kwa hifadhi na walitoa mapendekezo yao lakini hayakufanyiwa kazi badala yake vikosi vilipelekwa.”

Naye Robert Kamakia, kutoka Shirika linalotetea haki za wafugaji (PALISED), ameiomba Serikali iondoe vikosi vya ulinzi na usalama wilayani humo, amedai vinasababisha kamata kamata ya wananchi, watetezi wa haki za binadamu na viongozi.

Amesema, vikosi hivyo vikiondolewa wananchi watakuwa na imani na Serikali pamoja na kutoa ushirikiano kwa hiari.

“Kulikuwa na kamata kamata Tarafa ya Loliondo, viongozi zaidi ya 20 walikamatwa na kufunguliwa kesi ya mauaji akiwemo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ngorongoro. Hili ni la kuangaliwa kwa jico la tatu ili wasiokuwa na hatia waachwe huru,” amesema Robert.

Serikali ya Tanzania imetenga eneo katika kijiji cha Msomera kwa ajili ya wananchi waliokubali kuhama Ngorongoro kwa hiari, huku ikisema itaendesha zoezi hilo kwa kufuata misingi ya haki za binadamu.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!