Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Biashara Vodacom yawazawadia mawakala wa usajili kupitia kampeni ya ‘Loyalty Program’ nchini kote
Biashara

Vodacom yawazawadia mawakala wa usajili kupitia kampeni ya ‘Loyalty Program’ nchini kote

Spread the love

KAMPUNI ya Vodacom Tanzania imewazawadia mawakala wa usajili wa (Freelancer) ya jiko la gezi na mtungi wake ikiwa ni sehemu ya kampeni yake ya ‘Loyalty Program’ ambayo inalenga kuboresha maslahi ya mawakala wa usajili nchini kote. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).  

Kampeni hiyo ya ‘Loyalty Program’ mbali na zawadi ya jiko la gesi na mtundi wake pia inatoa zawadi kama vile bima ya afya, pikipiki, luninga, simu za mkononi, magodoro, pesa taslimu na ikiwemo safari itakayogharamiwa kila kitu ya kwenda nchini Afrika ya Kusini mwezi Oktoba 2023.

Kupitia kampeni hiyo Vodacom imewazawadia mawakala wawili wa jijini Dar es Salaam ambao wamefanya vizuri katika shughuli zao za usajili na kujikusanyia pointi nyingi, mawakala hao ni Goodluck Clement na Mathias Lutumbi.

Msimamizi wa Mauzo wa Vodacom Tanzania, Iddy Chitanda (kulia) akimkabidhi wakala wa usajili Goodluck Clement (kushoto) zawadi ya jiko la gesi na mtungi wake baada ya kujikusanyia pointi nyingi kwa kusajili wateja wapya wengi na wateja hao kununua salio na vifurushi kupitia M-Pesa.

Msimamizi wa Mauzo wa Vodacom Tanzania, Iddy Chitanda (kulia) akimkabidhi wakala wa usajili Mathias Lutumbi (kushoto) zawadi ya jiko la gesi na mtungi wake baada ya kujikusanyia pointi nyingi kwa kusajili wateja wapya wengi na wateja hao kununua salio na vifurushi kupitia M-Pesa.

Msimamizi wa Mauzo wa Vodacom Tanzania, Iddy Chitanda (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na mawakala wa usajili wa kampuni hiyo Mathias Lutumbi (kulia) na Goodluck Clement (kushoto) mara baada ya kuwakabidhi zawadi za majiko ya gesi na mitungi yake baada ya kujikusanyia pointi nyingi kila baada ya mteja mpya aliyemsajili akinunua salio na bando kwa M-Pesa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Orb of Destiny kutoka Meridianbet kasino ushindi kwa njia 14  

Spread the love  ORB of Destiny ni mchezo wa sloti kutoka kwa...

Biashara

Jiandalie Strawberry Cocktail yako nyumbani huku unacheza kasino 

Spread the love  UTAANDAA matunda yako unayotaka kutumia unaweza kutumia Strawberry, Cantaloupe...

Biashara

420 Blaze It chimbo jipya la kuchota mihela Meridianbet kasino 

Spread the love  JE, umewahi kucheza mchezo wa droo wenye droo 10?...

Biashara

Exim yawainua kiuchumi wanawake wajasiriamali kupitia mpango wa WEP

Spread the love  BENKI ya Exim kupitia Mpango wake wa Kuwawezesha Kiuchumi...

error: Content is protected !!