Tuesday , 26 September 2023
Home Kitengo Michezo Yanga malizeni ugomvi na Fei Toto – Rais Samia
MichezoTangulizi

Yanga malizeni ugomvi na Fei Toto – Rais Samia

Spread the love

 

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ameitaka klabu ya Yanga kumaliza tofauti zake na mchezaji wake wa kutumainiwa Feisal Salum ‘Fei Toto.’ Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea). 

Akizungumza katika hafla ya kupongeza timu hiyo, kwa kushinda mchezo wake wa pili wa fainali Jumamosi iliyopita, nchini Algeria, leo Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Samia alisema, hafurahishwi kuona Yanga inaendeleza mgogoro na mchezaji wake.

“Klabu ya Yanga ni kubwa sana. Ni aibu kuendeleza magomvi na wachezaji wake. Naomba hili la Fei Toto, kalimalizeni na nasubiria mrejesho,” alisisitiza Rais Samia.

Fei Toto aliondoka Yanga kuanzia mwishoni mwa mwaka jana, baada ya kudai kuwa anahitaji maslahi zaidi, akavunja mkataba kwa kuweka kiasi cha Sh. 112 milioni kwenye akaunti ya klabu hiyo, kwa lengo la kuvunja mkataba wake.

Hata hivyo, Kamati ya Sheria Hadhi za Wachezaji iliyopo chini ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ilieleza kuwa mchezaji huyo bado ni mali ya Yanga kwa kuwa hakufuata taratibu za kuvunja mkataba wake.

Kwa muda sasa, mchezaji huyo amekuwa akihaha kutaka kuondoka ndani ya klabu hiyo, lakini juhudi zake zimekuwa zikigonga mwamba, baada ya vyombo vinavyoongoza michezo kuelekeza kuwa Feisal Salim, anapaswa kufanya majadiliano na klabu yake, kabla ya kuvunja mkataba

Haijaweza kufahamika mara moja, iwapo Fei Toto atarejea Yanga au ataruhusiwa kuondoka. Ombi la Dk. Samia kutaka Yanga kumalizana na Fei Toto, halikueleza pande hizo mbili kuchukua hatua gani.

Katika hafla hiyo, viongozi mbalimbali wa michezo, akiwamo Ledger Tenga, mwenyekiti wa Baraza la Michezo la taifa (BMT); Wallace Karia, rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF); mhandishi Hersi Said; Murtaza Mangungu, Mwenyekiti wa Simba na Ghalib Said Mohamed, mfadhili mkuu wa Yanga, walihudhuria hafla hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

BiasharaMichezo

Piga pesa kupitia Derby ya London Kaskazini kwa kubadhiri na Meridianbet

Spread the love NAJUA umesikia na unazijua Derby nyingi kutoka jiji la London,...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme wang’oa vigogo TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewahamisha waliokuwa vigogo wa...

BiasharaMichezo

Wikiendi hii ushindi upo Meridianbet na si kwingine

Spread the love USHINDI huu ni wako mteja wa Meridianbet kama mechi...

error: Content is protected !!