Friday , 29 March 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Rais Kagame afanyia mabadiliko makubwa jeshi, usalama wa taifa
Kimataifa

Rais Kagame afanyia mabadiliko makubwa jeshi, usalama wa taifa

Spread the love

RAIS wa Rwanda, Paul Kagame amefanye uteuzi wa wakuu wapya wa kijeshi na kijasusi nchini mwake, katika mojawapo ya mabadiliko makubwa kabisa ya kiusalama yaliyofanywa na kiongozi huyo, katika miaka ya hivi karibuni. Anaandika Mwandishi Wetu…(endelea).

Katika mabadiliko hayo, Juvénal Marizamunda, sasa ndiye waziri mpya wa ulinzi wa Rwanda; huku Luteni Jenerali Mubarakh Muganga, akifanywa kuwa mkuu mpya wa majeshi (RDF).

Bwana Marizamunda, anachukua nafasi ya Meja Jenerali Albert Murasira. Kabla ya uteuzi huo, Marizamunda alikuwa Mkuu wa Jeshi la Magereza.

Luteni Jenerali Muganga, aliyechukua nafasi ya Jenerali Jean Bosco Kazura, alikuwa kamanda mkuu wa jeshi la ardhini.

Naye Meja Jenerali Vincent Nyakarundi, ambaye hapo awali alikuwa mkuu wa upelelezi wa kijeshi, amechukua nafasi ya Luteni Jenerali Muganga kama kamanda mkuu wa jeshi la ardhini.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kiusalama wanasema, haya ni mabadiliko makubwa ambayo rais Kagame ameyafanya katika vyombo vya ulinzi na usalama katika siku za karibuni.

“Haya siyo mabadiliko yanayotokea mara kwa mara katika jeshi la Rwanda, kwamba waziri wa ulinzi anabadilishwa kabla hajatumikia miaka mitano?

“Kwamba, mkuu wa majeshi anabadilishwa kabla hajatimiza miaka minne kwenye wadhifa huo na wanaondolewa kwa wakati mmoja? Hapana,” ameeleza John Rudahigwa, raia wa Rwanda aishiye jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, mpaka sasa, siyo Rais Kagame wala wasaidizi wake, walioeleza sababu ya mabadiliko haya.

Katika tangazo lililotolewa na ofisi ya rais Jumatatu usiku, na katika mabadiliko kama hayo ambayo yamewahi kutokea, wakati mwingine Rais Kagame mwenyewe, ndiye aliyekuwa akieleza sababu ya kufanya hivyo.

Rais wa Rwanda Paul Kagame

Kwa mujibu wa tangazo la mabadiliko hayo, Kanali Francis Regis Gatarayiha, ameteuliwa kuwa kaimu mkuu wa ujasusi wa kijeshi, huku Jean Bosco Ntibitura – aliyekuwa aliyekuwa mkuu wa majeshi ya Rwanda – akiteuliwa kuwa mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa katika Huduma ya Kitaifa ya Ujasusi (NISS).

Brigedia Jenerali Evariste Murenzi aliteuliwa kuwa mkuu wa jeshi la Magereza, akichukua nafasi ya Marizamunda.

Meja Jenerali Alex Kagame amechukua wadhifa wa kamanda wa operesheni za kijeshi nchini Msumbiji. Kabla ya uteuzi huo, Meja Jenerali Kagame alikuwa mkuu wa kitengo cha jeshi chenye nguvu maarufu kama ‘Republican Guard.’

Aidha, Kanali Théodomir Bahizi amekabidhiwa kusimamia masuala ya vita nchini Msumbiji, ambako tangu Julai 2021, taifa hilo mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, limetuma wanajeshi na polisi nchini Msumbiji, kwa ombi la serikali ya nchi hiyo, kupambana na watu wenye itikadi kali.

Wanamgambo hao wanaodai kuwa ni Waislamu wanaoungwa mkono na makundi yanayotuhumiwa na ugaidi, walitangaza kuteka maeneo mengi ya jimbo la Cabo Delgado, kaskazini mwa nchi Msumbiji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanaye rais jela miaka miaka 6 kwa dawa za kulevya

Spread the loveMwanawe rais wa zamani wa Guinea-Bissau amehukumiwa kifungo cha miaka...

Habari za SiasaKimataifa

Faye aahidi kuongoza kwa unyenyekevu, wagombea wenzie wakubali yaishe

Spread the loveMgombea wa upinzani Senegal, Bassirou Diomaye Faye anajiandaa kuwa rais...

error: Content is protected !!