March 5, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Viziwi wapewa elimu ya kilimo

Mashine ya kuvutia maji kwaajili ya umwagiliaji

Spread the love

CHAMA cha Maendeleo ya Kilimo kwa Viziwi Tanzania (CHAMAKIVITA) kimejipanga kutoa elimu kwa viziwi ili kuwawezesha kulima kilimo cha kisasa, anaandika Dany Tibason.

Kelvin Nyema ambaye ni kiongozi mtendaji wa chama hicho alisema kuwa chama hicho kimejipanga kutoa elimu kwa viziwi ambao ni wakulima kwa lengo la kuwaodolea changamoto wanazokumbana nazo.

Nyema amesema licha ya viziwi kujihusisha na kilimo, lakini wamejikuta wakilima bila kuwa na tija kutokana na kutokuwa na elimu ya kuhusu kilimo na kutokujua msimu halisi.

Amesema kutokana na changamoto mbalimbali za kimawasiliano viziwi wengi ambao wamekuwa hawajui namna bora ya kulima kilimo cha kisasa ikiwa ni pamoja na kutofahamu majira halisi ya kilimo.

“Tumelazimika kuanzisha chama cha maendeleo ya kilimo kwa viziwi Tanzania kwa lengo la kuwakwamua viziwi ambao wanajihusisha na kilimo,wakulima wengi ambao ni viziwi wanalima lakini kilimo chao bado ni duni.

“Kutokana na changamoto hizo kwa sasa tutatoa elimu kwa wakulima ambao ni viziwi kwa lengo la kuwafanya wakulima hao walime kilimo cha kisasa na kutumia pembejeo ambazo zinaendana na msimu wa kilimo.

“Kama viziwi watapatiwa elimu bora ya kilimo wataweza kulima kilimo bora na kuwaondolea dhana kwamba kundi hilo ni wategemezi, tunatazamia washiriki 300 watapatiwa elimu.

error: Content is protected !!