Sunday , 25 February 2024
Home Habari Mchanganyiko Madereva daladala Ubungo wamaliza mgomo
Habari Mchanganyiko

Madereva daladala Ubungo wamaliza mgomo

Spread the love

Madereva wa Daladala  kituo cha  Simu 2000, Manispaa ya Ubungo jijini Dar es salaam,  wamekubali kumaliza mgomo waliouanza mapema leo asubuhi kutokana watendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kutoa agizo la kupanda kwa bei ya Ushuru kutoka Sh  500 hadi  Sh 1000, anaandika Irene David.

Mstahiki Meya Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob, ameagiza kurudi kiasi kilikile cha shilingi 500 kwa siku kwa kila daladala kwa kuwa baraza la madiwani halikuongeza kiasi hicho.

“Nimesikitishwa na watendaji wetu wa Halmashauri kutuingiza kwenye mgogoro na watumiaji wa huduma hii bila sababu za msingi, kwamba wana amka na kuongeza ushuru kutoka kiasi cha sh 500 mpaka sh 1000 bila kujua kuwa sheria hairuhusu jambo hilo.” Amesema Meya.

Meya amesema hatua kali za kinidhamu zitatolewa  kwa waliopandisha kiasi hicho kwa kuwa baraza la madiwani halikuongeza kiasi hicho kama sheria ilivyo na baadae mabadiliko hayo kusainiwa na Waziri wa  Ofisi ya Rais Tawala za Mkoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) ndipo ianze kutumika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

25 wafariki dunia katika ajali Arusha

Spread the loveWatu 25 wamefariki dunia papo hapo mkoani Arusha katika ajali...

Habari Mchanganyiko

“Jamii ielimishwe faida za uhifadhi”

Spread the loveWIZARA ya Maliasili na Utalii imesema ili kukabiliana na migongano...

Habari Mchanganyiko

Shahidi aeleza Nathwani alivyomshambulia jirani yake

Spread the loveSHAHIDI ambaye ni fundi Seremala, Dominic Mpakani (43) ameileza mahakama...

Habari Mchanganyiko

DCEA, TAKUKURU waunganisha nguvu kupamba na dawa za kulevya, rushwa

Spread the love  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya...

error: Content is protected !!