March 8, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge Chadema atinga uraiani

Wabunge Ester Bulaya na Halima Mdee

Spread the love

HATIMAYE mbunge wa Bunda (Chadema), Ester Bulaya amepata dhamana baada ya kushikiliwa na Polisi kanda maalum ya Tarime na Rorya kwa amri ya Mkuu wa wilaya ya hiyo Glorious Luoga, anaandika Mwandishi Wetu.

Kabla ya kupata dhamana leo hii, wanachama wa Chadema kutoka maeneo mbalimbali mkoani Mara ikiwamo jimboni kwake, walifurika kituo cha polisi.

Kutokana na wingi wa wananchi hao wakiongozwa na Mbunge wa Tarime vijijini, John Heche, polisi wameonekana kuweka ulinzi mkali.

mwishoni mwa wiki, Bulaya alikamatwa na jeshi la Polisi akiwa katika Hotel ya Kifa Best Point Wilayani Tarime akidaiwa kujiandaa kutaka kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.

Kamanda wa polisi Tarime/Rorya Kamishina Msaidizi Mwandamizi Henry Mwaibambe alisema Bulaya hakutakiwa kushiriki katika mkutano wa Ester Matiko (Chadema), ambaye ni mbunge wa Tarime mjini

error: Content is protected !!