July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vituo vya ukaguzi mabasi ya umma vyaandaliwa

Mabasi ya abilia

Spread the love

SERIKALI kupitia Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani limeandaa utaratibu wa kuwa na vituo maalum vya ukaguzi vya mabasi ya umma. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo tarehe 23 Aprili 2019 bungeni na Hamad Masauni, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani alipokuwa akijibu swali la Rose Tweve (CCM).

Katika swali lake, Rose alitaka kujua ni lini serikali itaanza utaratibu wa kuwa na vituo maalum vya ukaguzi vya mabasi ikiwemo daradara?

Masauni amesema, vituo hivyo vitakuwa vituo vikuu vya mabasi yote katika kila mkoa, ambapo mabasi ya abiria hukaguliwa kabla ya kuanza safari na pale yanapofika mwisho wa safari.

Amesema, ukaguzi wa pembezoni mwa barabara ambao huhusisha mabasi ya daladala na vyombo vingine vya moto, hufanyika katika vituo vya ukaguzi maalum ambavyo vipo katika barabara kuu na katika barabara zingine za miji na majiji.

Amesema, Sheria ya Usalama Barabarani, Sura ya 168 iliyorejewa 2002 kifungu 81, kinampa uwezo Askari Polisi kulisimamisha gari lolote barabarani au sehemu yoyote anapolitilia shaka na kulikagua.

error: Content is protected !!