April 14, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Dk. Mwakyembe atonesha vidonda vya Azory

Spread the love

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, amepuuza kilicho cha muda mrefu cha wadau wa habari nchini cha kutaka kuelezwa mahali aliko, mwandishi wa gazeti la Mwananchi, Azory Gwanda. Anaripoti Mwandishi Wetu kutoka Dodoma … (endelea).

Akizungumza bungeni leo Jumanne, Dk. Mwakyembe, ametaka kupuuzwa kwa watu wanaotaka ripoti kamili ya kupotea kwa Azory. Alikuwa ahitimisha mjadala wa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha ujao wa fedha.

Mteule huyo wa Rais John Magufuli, amedai kushangazwa kwake na wanaofuatilia mahali aliko Gwanda, na kuongeza, “kama kupotea, waliopotea wako wengi.”

Azory Gwanda ametoweka katika mazingira ya kutatanisha tokea tarehe 21 Novemba 2017. Mpaka sasa, hakua ripoti yoyote iliyotolewa kutoka chombo chochote cha ulinzi na usalama juu ya kupotea kwake.

Mke wake, Anna Pinoni, alinukuliwa akisema, “…watu wapatao wanne, wakiwa kwenye gari aina ya Toyota Land Cruiser, yenye rangi nyeupe, walimchukua mume wake (Azory Gwanda), kutoka katikati ya mji huo, mahali ambapo hupendelea kukaa.

“Kwamba, aliporudi nyumbani alikuta vitu vimezagaa, ishara kuwa waliipekua nyumba yao.”

Mwandishi huyo mahiri wa habari, alikuwa akiishi na kufanyia shughuli zake katika mji mdogo wa Kibiti, mkoani Pwani.

Alikuwa mmoja wa waaandishi wa kwanza kabisa wa habari, kuripoti kwa kina, juu ya mfululizo wa mauwaji, yaliyokuwa yakitekelezwa katika eneo hilo.

Akitetea hoja yake ya kutaka wananchi kipuuza taarifa za kumtafuta mwandishi huyo, Dk. Mwakyembe amesema, kuna watu wengi wamepotea katika eneo hilo, wakiwemo vongozi wa serikali.

Ameapa kuwa “serikali itaendelea kuwadhibiti watu wanaokiuka utoaji wa maoni, kwa kuwa hakuna uhuru usiokuwa na mipaka.” Hakufafanua.

Hata hivyo, baadhi ya wachambuzi wa kisiasa, wanaitafsri kauli yake kuwa yawezekana kwa kuwa serikali ina mikono mirefu, inafahamu ya kupotea kwa mwandishi huyo.

error: Content is protected !!