October 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Vipaumbele 10 vya serikali 2020/21 hivi hapa

Spread the love

SERIKALI imeweka vipaombele 1 vya miradi ya maendeleo kwa mwaka 2020/2021 ili kuhakikisha uchumi unakuwa kwa kasi. Anaripoti Faki Sosi, Dar es Salaam … (endelea).

Viapumbele hivyo vimeanishwa leo tarehe 11 Juni 2020 na Dk. Philip Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango bungeni jijini Dodoma wakati akieleza Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2020/21.

Vipaumbele hivyo ni:-

Ujenzi wa Reli ya Kati ya Standard Gauge

Serikali imetenge Sh. trilioni 2.1 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kipande cha Dar es Salaam – Morogoro (km 300); kuendelea na ujenzi wa kipande cha Morogoro – Makutopora (km 422); kuendelea na taratibu za upatikananaji wa mkandarasi kwa vipande vya Makutopora – Tabora (km 376.5).

Pia Tabora – Isaka (km 162) na Isaka – Mwanza (km 311.3); kuendelea na taratibu za upatikanaji wa washauri elekezi na utoaji wa ardhi kwa vipande vya Tabora – Kigoma (km 411), Kaliua – Mpanda – Karema (km 320), Uvinza – Msongati (km 240) na Isaka – Rusumo (km 371).

Mradi wa Kufua Umeme wa Maji wa Julius Nyerere – MW 2,115

Kwenye mradi huu, kazi zitakayofanyika ni kuendelea na ujenzi wa bwawa; ujenzi wa njia kuu za kupitisha maji; ujenzi wa eneo la kufunga mitambo ya kufua umeme; na ujenzi wa kituo cha kusafirisha umeme ambapo shilingi trilioni 1.44 fedha za ndani zimetengwa.

Kuboresha Shirika la Ndege Tanzania

Sh. 450 bilioni 450, fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kununua ndege moja ya mizigo na moja ya abiria aina ya Boeing 787-8 Dreamliner, kukamilisha malipo ya ndege mbili aina ya Airbus A220–300, kununua vifaa vya kuhudumia ndege na abiria viwanjani, kulipa madeni ya Shirika na kukarabati Hangar za KIMAFA (KIA) na JNIA.

Mradi wa Makaa ya Mawe Mchuchuma

Shughuli zilizopangwa kwenye mradi huu ni kuhakiki mali za wananchi watakaopisha mradi pamoja na uperembaji na tathmini ya mradi ambapo Sh. 110 milioni, fedha za ndani zimetengwa.

Kiwanda cha kufua chuma cha Liganga

Shughuli zilizopangwa ni kuhakiki mali za wananchi watakaopisha mradi pamoja na uperembaji na tathmini ya mradi ambapo Sh. 120 milioni, fedha za ndani zimetengwa.

Ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima (Uganda) hadi Tanga (Tanzania)

Shughuli zitakazotekelezwa ni pamoja na kukamilisha majadiliano ya mikataba ikiwemo ya Nchi Hodhi na Wawekezaji, mkataba wa ubia, mkataba wa bandari, mkataba wa pango la ardhi na kulipa fidia ambapo shilingi bilioni 1 fedha za ndani zimetengwa.

Mradi wa kuchakata na kusindika gesi asilia – Lindi

Kwenye mradi huu, shughuli zitakazotekelezwa ni kuendelea na tafiti mbalimbali za kitaalam pamoja na majadiliano ya mradi. Sh. 2.6 bilioni, fedha za ndani zimetengwa.

Uanzishwaji wa Kanda Maalum za Kiuchumi

Jumla ya Sh 5 bilioni, fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya uendelezaji wa kanda maalum za kiuchumi. Shughuli zitakazotekelezwa ni:

Eneo Maalum la Uwekezaji Bagamoyo: kukamilisha uandaaji wa nyaraka za kisheria kwa ajili ya mradi; kukamilisha taratibu za umilikishaji ardhi katika eneo lililolipiwa fidia; kufanya usanifu wa kina na ujenzi wa miundombinu wezeshi katika eneo la kituo cha Teknolojia Bagamoyo; kujenga barabara katika eneo lililojengwa viwanda 11, ambapo shilingi bilioni 4 fedha za ndani zimetengwa. 

Eneo Maalum la Uwekezaji la Ukanda Huru wa Bandari ya Mtwara: kujenga jengo la Kituo cha Pamoja cha Huduma na uzio ambapo shilingi bilioni 1.5 fedha za ndani zimetengwa.

Kituo cha Biashara na Huduma Kurasini: shilingi bilioni 2.2 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya kulipa fidia kwa wakazi watatu ambao awali nyumba zao hazikufanyiwa thamini; kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya kuliendeleza eneo na tathmini ya athari za kijamii na mazingira.

Shamba la miwa na Kiwanda cha Sukari Mkulazi (I na II)

Shughuli zitakazotekelezwa ni: Mkulazi I – kuendelea na upanuzi wa kitalu cha miwa kufikia hekta 250 na maandalizi ya ujenzi wa kiwanda; Mkulazi II – kuzalisha tani 2,300 za sukari; kuendelea na ujenzi wa mifumo ya umwagiliaji, vyanzo vya maji na barabara katika eneo la shamba; na ujenzi wa mabwawa madogo sita (6) yenye mita za ujazo 250,000 na makubwa matatu (3) yenye mita za ujazo 1,000,000.

Kusomesha kwa wingi wataalam kwenye Fani na Ujuzi Adimu.

Kuendelea kugharamia mafunzo kwa wanafunzi katika fani mbalimbali zinazohitajika kwa ajili ya kuchochea maendeleo ya viwanda na watu nchini.

Fani hizo ni pamoja na mafuta na gesi, afya hususan udaktari bingwa kwa ngazi za uzamili na uzamivu katika nyanja zote za magonjwa ya upasuaji wa ubongo na mishipa ya fahamu, upandikizaji figo, ini na uboho (bone marrow), tiba za ndani za moyo, na uhudumiaji wa wagonjwa wa dharura na mahututi.

error: Content is protected !!