Thursday , 7 December 2023
Home Kitengo Maisha Afya Mapambano ya corona Tanzania, IMF yatoa msamaha wa mabilioni
AfyaHabari za Siasa

Mapambano ya corona Tanzania, IMF yatoa msamaha wa mabilioni

Spread the love

DK. John Magufuli, Rais wa Tanzania amesema, atamwandikia barua Kristalina Georgieva, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha za Kimatiafa (IMF ), kwa ajili ya kulipongeza shirika hilo, kwa kutambua juhudi za taifa hilo katika kukabiliana na mlipuko wa virusi vya corona (Covid-19). Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Rais Magufuli amesema hayo leo Alhamisi tarehe 11 Juni 2020 wakati akihutubia katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya lami kwenye mji wa Serikali, ulioko Mtumba jijini Dodoma na jingo la Mamlaka ya barabara za mjini na vijijini (Tarura).

Kiongozi huyo wa Tanzania amesema barua hiyo kwa ajili ya kuipongeza  IMF ataiandika leo baada ya IMF kuisamahe nchi hiyo kodi ya Dola za Marekeani milioni 14.3.

“Nimepanga leo nitamuandikia barua mkurugenzi mkuu wa IMF kwa niaba ya Watanzania kuwapongeza kwamba wametambua juhudi zetu,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo baada ya Bodi ya Wakurugenzi ya IMF kuidhinisha msamaha wa kodi  ya mikopo ya Tanzania katika shirika hilo, kiasi cha Dola za Marekani 14.3 Milioni (sawa na Sh.32.9 bilioni)

Rais Magufuli amesema bodi hiyo iliidhinisha msamaha huo leo Alhamisi.

Amesema, fedha hizo zitatumika katika mapambano dhidi ya corona.

“Leo ninapozungumza tumepata fedha za masamaha, bodi ya wakurugenzi IMF imeidhinisha leo dola 14.3 milioni za msamaha wa kodi ya madeni tuliyokuwa nayo, na kwa sababu tulipambana vizuri sana na ugonjwa wa corona, msamaha huo umekuja wakati muafaka,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema, msamaha huo umekuja wakati muafaka na kwa kuwa Tanzania ilipambana vizuri dhidi ya janga hilo.

Kwa mara ya kwanza nchi ya Tanzania ilitangaza mgonjwa wa cha kwanza wa corona tarehe 16 Machi 2020.

Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kukabiliana na mlipuko wa corona ni, kuunda kamati maalumu iliyoongozwa na Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu na Kikosi Kazi cha kudhibiti na kukabiliana na janga la Corona.

Kutenga hospitali na maeneo maalumu kwa ajili ya kutoa huduma kwa watu walioambukizwa ugonjwa huo, kufunga kwa muda shule za awali, msingi na sekondari,  vyuo vya kati na vyuo vikuu, kusitisha shughuli za michezo, mikusanyiko, warsha na makongamano.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

error: Content is protected !!