Thursday , 13 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Viongozi wanaotumia madaraka vibaya waonywa
Habari Mchanganyiko

Viongozi wanaotumia madaraka vibaya waonywa

Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama
Spread the love

VIONGOZI mbalimbali wametakiwa kutokutumia madaraka yao vibaya kwa ajili ya kujiufaisha wenyewe badala yake watambue kuwa nafasi walizonazo ni kwaajili ya kuwatumikia watu wengine na kwa faida ya jamii na taifa kwa ujumla. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Ushauri huo umetolewa na askofu wa kanisa la The Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT) Jimbo la Dodoma, Meshack Temba wakati wa ibada maalumu ya kuwasimika wachungaji wa kanisa la mahali wa kanisa hilo ambao ni mchungaji kiongozi Daud Masaghaa, wa kanisa la FPCT Chang’ombe, Makamu nchungaji kiongozi Elia Timothy, FPCT Chamwino mjini, Katibu Nelson Maganga,Mkamu Katibu John Piusna Mtunza hazina Jeremiah Maisel.

Askofu Temba amesema kuwa anakerwa na viongozi ambao wamekuwa wakitumia madaraka yao vibaya ikiwa ni pamoja na kuwanyanyasa waliopo chini yao na kujirimbikizia mali badala ya kuwa msaada kwa wale wanaowaongoza.

Amesema kuwa kiongozi yoyote awe wa Kiroho au Kiserikali ni lazima atambue kuwa nafasi aliyonayo ni ya kuwatumikia wananchi au wale anaowaongoza na siyo kujitunisha na kuvimba na kuona waliopo chini yake ni kama takataka. “Kiongozi mwema ni yule ambaye anakuwa karibu na watu, mwenye kujua shida za watu na kuzitafutia ufumbuzi na siyo kujirimbikizia mali na kuwa mbali na wale anaowaongoza na kwa kufanya hivyo ni kukosa kuelewa nia dhabiti ya kupewa uongozi.

“Kiongozi yoyote ambaye si mtu wa watu na hajali matatizo ya watu kwa vyovyote vile ni lazima atakuwa fisadi na mtu ambaye hawezi kujua matatizo ya watu wake na kuyatatua na kiongozi wa aina hiyo ni bora akaachia ngazi ili aweze kufanya kazi nyingine ambazo si za kuiongozi” amesisitiza Askofu Temba.

Katika hatua nyingine amewakemea watumishi wote ndani ya serikali na ndani ya dini mbalimbali ambao wanakuwa wachochezi wa migogoro au kuzusha migogoro na kutaka tabia hizo zikome mara moja kwa maelezo kuwa migogoro haiwezi kuwa na ustawi katika nchi au katika mahali popote pa kazi.

“Hatuwezi kuwa na viongozi ambao wanachochea migogoro na kiongozi yoyote ambaye ni msababishi wa migogoro katika eneo lake la kazi hafai kuendelea na kazi hiyo na badala yake anatakiwa kuachia ngazi mara moja na kutafuta kazi nyingine ya kufanya” amesisitiza Askofu Temba.

Kwa upande wa viongozi waliosimikwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi wamesema kuwa watasimamia kiapo chao na maadili ya utumishi huku wakifanya kazi kwa kuzingatia misingi na shiria za nchi kwa kutambua kuwa wao wapo kwa ajili ya kusaidia watu kimwili na Kiroho.

Mchungaji Kiongozi Daudi Msaghaa amesema kuwa yeye kwa nafasi yake atafanya kazi ya Mungu kwa kuzingatia misingi ya imani ya Kikristo na kuheshimu dini nyingine lakini zaidi kuwahakisha anatoa huduma kwa watu wote bila kuwa na ubaguzi.

Naye mchungaji kiongozi msaidizi Elia Timothy ameeleza kuwa ataifanya kazi hiyo kwa kumtanguliza Mungu ikiwa ni pamoja na kutafuta hekima na busara kutoka kwa watangulizi wake huku akieleza kuwa msingi wake mkubwa ni kusimamia neno la Mungu na kufuata sheria za nchi. Salma.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Deni la Serikali lafikia trilioni 91

Spread the loveWaziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema hadi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

GGML yaahidi kuendelea kushirikiana na UDSM kudhamini tafiti, ubunifu

Spread the loveKAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imeahidi kuendelea kushirikiana...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Marekani yasaka fursa uwekezaji sekta ya nishati Tanzania

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko amekutana...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

RC Chalamila: Wasanii wanamchango mkubwa katika maendeleo ya Taifa

Spread the loveMkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila ametoa...

error: Content is protected !!