KAMPUNI pamoja na taasisi mbalimbali ambazo ni wateja wa Benki ya Taifa ya Biashara ya (NBC), sasa wanaweza kupata uzoefu mpya wa huduma za kibenki kupitia huduma ya NBC Connect, ikiwa ni ingizo jipya la huduma za kibunifu za kidigitali. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

NBC Connect, ni huduma ya kisasa ya kidigitali, ambayo huwezesha huduma salama za kibenki ambazo huweza kufanyika sehemu yoyote, muda wowote kwa njia ya mtandao. Huduma hii ni sehemu ya mchango wa benki katika kuunga mkono jitihada za Serikali za kuongeza ujumuifu katika huduma za kifedha.
Uzinduzi wa huduma ya NBC Connect kanda ya Ziwa, ni wa pili baada ya uzinduzi kwa kanda ya nyanda za juu kusini uliofanyika jijini Mbeya mwezi uliopita.

Kupitia NBC Connect, wateja wenye makampuni na taasisi mbalimbali zilizopo mkoa wa Mwanza na maeneo ya jirani, watapata fursa na uwezo wa kufanya miamala yao ya kifedha kwa urahisi zaidi na kupata uzoefu mpya katika kupata huduma za kibenki.
Akizungumza katika uzinduzi huo mkoani Mwanza, Mkuu wa kitengo cha wateja wa kimataifa wa benki ya NBC Wilson Nkuzi amesema huduma hiyo itawapa wateja uwezo wa kufanya miamala kirahisi ikiwa ni pamoja na malipo ya ndani na nje ya nchi, malipo ya Serikali pamoja na malipo kwa mkupuo bila kuchukuaa muda kwa kutumia simu au kompyuta.

Amesema wateja pia wataweza kupata taarifa za miamala waliyofanya popote pale walipo pasipo kulazimika kwenda benki.
“NBC Connect imetengenezwa kwa teknalojia ya kisasa na yenye usalama wa hali ya juu ambayo imezingatia na kutoa kipaumbele kwenye usiri wa taarifa za mteja. Ubunifu wa huduma hiyo huakikisha taarifa za kifedha za wateja zinalindwa wakati wote.

“Tunafuraha kutambulisha NBC Connect kwa wakazi wa kanda ya ziwa na maeneo ya jirani. Mfumo huu wa kibenki wa kidigitali ni uthibitisho wa dhamira ya kuwapatia wateja wetu huduma bora za kibenki ambazo ni rahisi, salama, na zinazofaa na kukidhi mahitaji ya wateja. NBC Connect itawawezesha wateja wetu kufanya huduma zakibenki popote pale, wakati wowote, na kufurahia huduma hizo bila matatizo,” amesema
Pamoja na huduma rahisi na za kisasa, NBC Connect itatoa usaidizi binafsi kwa wateja kupitia kituo chake cha huduma kwa wateja ambapo mameneja wake katika kituo cha huduma kwa wateja wanapatikana ili kuwasaidia wateja kulingana na mahitaji yao nakutoa mwongozo wa jinsi ya kutumia jukwaa hilo kwa ufanisi.
Amesema ili kusherehekea uzinduzi wahuduma hiyo jijni Mwanza, Benki ya NBC itatoa maelezo ya kina juu ya huduma hiyo na kwa wateja watakaojiandikisha na kujiunga na huduma hiyo ili kuwapa uelewa mpana wa namna ya kuitumia na kufurahia huduma hiyo.

“Tunawaalika wateja wetu wote wa kanda ya Ziwa na maeneo ya jirani wajionee urahisi na usalama wa NBC Connect. Ni huduma ambayo inaleta mapinduzi mapya katika namna ambavyo huduma za kibenki zinatolewa. Tuna uhakika kuwa wateja wetu watafaidika nayo kwa kiasi kikubwa , “ameongeza.
Kwa upande wake Katibu tawala wa mkoa wa Mwanza, Bulandya Elikana aliishukuru Benki ya NBC kwa ubunifu wao mzuri na kuwahimiza wateja kutumia mfumo huo mpya wa kibenki ili kurahisisha shughuli zao za kila siku.
“Uzinduzi wa NBC Connect kanda ya Ziwa unawakilisha mpango mkakati wa upanuzi wa benki ya NBC ili kuwafikia wananchi wengi zaidi na kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi.
“Benki ya NBC inasifika kwa dhamira yake kubwa ya kuwajibika kwa jamii, ikiwa ni pamoja na kusaidia jamii kupitia mipango mbalimbali, kama vile Mbio za Kimataifa za NBC Dodoma Marathon zinazohamasisha matibabu ya saratani ya shingo ya kizazi, msaada wa afya ya uzazi kupitia kliniki zinazotembea, programu za elimu ya kifedha, uwezeshaji wa vijana. kupitia udhamini wa Ligi Kuu ya NBC, hakika napongeza juhudi hizi zinazofanywa na NBC” alisema.
Leave a comment