Saturday , 22 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Fomma yakumbuka wanafunzi wa Bugiri wasioona
Habari Mchanganyiko

Fomma yakumbuka wanafunzi wa Bugiri wasioona

Spread the love

JAMII imetakiwa kujenga desturi ya kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingiramagumu kwa kuwapatia elimu na haitaji muhimu ya kibanadamu na siyo kuwanyanyasa na kuwanyanyapaa kutokana na hali zao za maisha walizonazo. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Ushauri huo umetolewa leo tarehe 21 Mei 2023 na Mwenyekiti wa Friends Of Mc Mwangata Assosiation (FOMMA)Dk.Gasper Kisenga  muda mfupi baada ya kukabidhi misaada mbalimbali ya kibinadamu kwa wanafunzi wa shule ya msingi ya Buigiri kata wilaya ya Chamwino ambayo utoa mafunzo kwa wanafunzi wasioona, wenye uoni afifu na watu wenye ulemavu wa ngozi.

Dk. Kisena amesema kuwa umoja huo umetoa msaada wa vyakula, vifaa nya shule dawa za meno, pamoja na kisimbuzi kwa ajili ya kuwafanya watoto hao kuwa na furaha kama walivyo watoto wengine ambao wanaishi katika maisha ya kawaida na wazazi wao.

“Tumekuja shuleni hapa kuwaona hawa watoto zetu ambao wanasoma shule ya msingi Buigiri ambayo ni shule kongwe iliyoanzishwa mwaka 1950 kwa ajili ya kuwafundisha watoto wenye matatizo ya kutokuona na wenye matatizo ya uoni afifu.

“Kwa mazingira ya kawaida watoto hao wanahitaji nao kuishi kama walivyo watoto wengini na wanahitaji kuoneswa upendo na kujaliwa kwa kupatiwa mahitaji muhimu ya kibinadamu kama ilivyo watoto wengine hivyo jamii, taasisi mbalimbali ione kuwa kuna umuhimu wa kuwajari na kuwapatia misaada mbalimbali ili kuwafanya kuwa katika hali ya kujiona kuwa nao ni sehemu ya watoto wengine ambao wanaishi maisha bora na mazuri” ameeleza Dk. Kisenga.

Aidha amewataka wazazi na walezi kutowaficha watoto wao wenye matatizo mbalimbali ya ulemavu wa aina yoyote na badala yake wanatakiwa kuwapeleka shuleni ili waweze kupatiwa elimu kama ilivyo kwa watoto wengini kwa maelezo kuwa kila mtoto bila kujali hali yake aliyonayo lakini anayo haki ya msingi ya kupata elimu.

Kwa upande wao wanafunzi wa shule ya wasioona Buigiri wamesema kuwa licha ya kuwa na ulemavu wa kutokuona lakini wamekuwa wakifanya vizuri kitaaluma na kushiriki michezo mbalimbali pamoja na shughuli mbalimbali za usafi wa mazingira kam walivyo wanafunzi wengine.

Ester Suve mwanafunzi wa darasa la sita shule ya wasioona Buigiri amesema kuwa wnafunzi hao licha ya kuwa hawaoni lakini wanahitaji nao kupendwa kujariwa na kuthaminiwa kwa kuwa tatizo walilonalo ni kutokuona lakini wanazo hakili timamu na ndiyo maana wanaweza kushiriki vyema katika masoma na kufanya vizuri pamoja na kushiriki michezo mbalimbali.

Naye mwalimu wa shule hiyo Wakati Joseph ameeleza kuwa licha ya wanafunzi hao kutokuwa na uwezo wa kuona lakini wamekuwa wakifanya kazi mbalimbali za mikono huku akieleza kuwa ni kati ya wanafunzi bora na wenye vipaji mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimba, kucheza mpira na kupiga gitaa.

Hata hivyo ameeleza kuwa kuna changamoto kadhaa ambazo shule inakutana nazo ikiwa ni pamoja na kukosekana vifaa vya kutosha vya watu wasioona ikiwa ni kukosekana kwa karatasi za maandishi ya nukta nundu,

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Askofu Wolfang Rais mpya TEC, Padri Kitima aula tena

Spread the loveBARAZA la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limetambulisha safu mpya za...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washiriki mbio za NBC Dodoma Marathon kutumia treni ya SGR kwenda Dodoma

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

Habari MchanganyikoTangulizi

Padre anayetuhumiwa mauaji ya Asimwe, asimamishwa

Spread the loveKanisa Katoliki Jimbo la Bukoba limemsimamisha kutoa huduma za kichungaji...

Habari Mchanganyiko

Upandaji miti uzingatie kuondoa umaskini kwa wananchi

Spread the loveKATIBU Tawala wa mkoa wa Morogoro Dk. Musa Ally Musa...

error: Content is protected !!