Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Viongozi wa dini watakiwa kulikomboa Taifa
Habari Mchanganyiko

Viongozi wa dini watakiwa kulikomboa Taifa

Kiongozi wa Kanisa la Jehova Mercy, Prophet Richard Magenge
Spread the love

KIONGOZI wa Kanisa la Jehova Mercy, lenye makao yake makuu Jijini Dodoma mtaa wa Swaswa Halisi, Prophet Richard Magenge amewataka viongozi wa Kiroho kufanya kazi ambayo inalenga kulikomboa taifa na roho za waumini wao. Anaripoti Dany Tibason, Dodoma … (endelea).

Mbali na hilo kiongozi huyo wa Kiroho amewataka viongozi ambao wamejitolea kumtumikia Mungu kufanya kazi zao kwa misimamo bila kuwa na hofu ya kibinadamu na walenge zaidi kufanya kazi ya ukombozi ambao una manufaa kwa jamii.

Alitoa kauli hiyo hivi karibuni katika ibada maalum ya kuwasimika wachungaji kumi wa kanisa hilo na kueleza kuwa kiongozi yoyote ambaye anamtumikia Mungu wa Kweli ni lazima asimamae imara kaitika kusema ukweli kwa lengo la kukomboa jamii na taifa kwa ujumla.

Katika maubiri yake Kiongozi huo ambaye amekuwa akifanya miujiza na utabiri kwa lengo la kuwaponya watu kwa nguvu ya Mungu alisema kazi ya Mungu haiitaji kufanywa kwa uzembe wala uoga badala yeke ni kuhakikisha inafanyika kwa nguvu ya Kimungu.

“Katika kuhakikisha kazi ya Mungu inafanyika mtumishi ambaye anafanya kazi ya kwa kuongopa maneno ya watu au lawama na kushindwa kusimamia ukweli ni kiongozi ambaye hajui wajibu wake na awezi kutumika katika shamba la Mungu.

“Katika mambo ambayo mimi siwezi kuogopa kufanya ni kusema ukweli ambao unalenga kuponya taifa, leo hii nawasimika viongozi kwa maana ya wachungaji nitashangaa sana kama kuna mtu ambaye atashindwa kuhubiri ukweli kwa lengo la kuongopa naneno ya watu.

“Mtumishi aliyetumwa na Mungu lazime aseme ukweli kwa kiongozoi yoyoye awe wa kiserikali, Kiroho ilimradi kufikisha ujumbe wa Mungu ambao anataka uwe Baraka kwa taifa lake,” alisema Prophet Magenge.

Katika hatua nyingine kiongozi huyo wa Kiroho aliwakemea viongozi wa serikali ambao wamekuwa wakikwamisha kazi ya Mungu kwa kuweka vikwazo mbalimbali hasa pale wanapotaka kupata maeneo ya kujenga nyumba za Ibada.

Alisema kazi ya Mungu haitakiwi kuchezewa kwani Mungu ni kiongozi mkubwa kuliko kiongozi yoyote Duniani na Mbinguni hivyo ni jambo jema kutulia na kusikiliza viongozi wa Kiroho wametumwa ujumbe gani kwa taifa husika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

ElimuHabari Mchanganyiko

Wanafunzi Nyamkumbu wanolewa na GGML kuhusu taaluma ya madini

Spread the loveZAIDI ya Wanafunzi 50 kutoka Shule ya Sekondari ya Wasichana...

error: Content is protected !!