Friday , 2 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Serikali kutoa mafunzo ya stakabazi ghalani
Habari Mchanganyiko

Serikali kutoa mafunzo ya stakabazi ghalani

Mahindi yakiwa shambani
Spread the love

HALMASHAURI ya wilaya ya Morogoro ina mpango wa kutoa elimu ya mfumo wa stakabadhi mazao ghalani kwa wakulima wilayani humo katika msimu wa kilimo 2018/19 ili kuwafanya kuweza kutumia maghala yaliyopo kwa manufaa tofauti na ilivyo kwa sasa. Anaripoti Christina Haule, Morogoro … (endelea).

Ofisa Kilimo wa wilaya hiyo Remijo Mpagama alisema hayo jana wakati Kituo cha Taarifa na maarifa cha Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP- Mtandao kilipokuwa kilitoa mrejesho waliofanya wa ufuatiliaji wa rasilimali za Umma (PETS) mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ambao ulibaini licha ya uwepo wa baadhi ya maghala ambayo yameisha kamilika ikiwemo la kata ya Mikese lakini hayatumiki ipasavyo bila sababu na kufanya wakulima kushindwa kunufaika

Mpagama alisema, kufuatia Halmashauri kubaini kuwa wakulima hawana uelewa wa mfumo wa stakabadhi ghalani wameshajipanga kutoa elimu hiyo kwa msimu wa kilimo 2018/19 ili kuwafanya waweze kunufaika kufuatia kwa sasa wakulima hao kutumia ghala la Mikese kwa kuhifadhia tu mazao yao.

Alisema, elimu hiyo itawanufaisha wakulima katika mambo mengi ikiwemo kuona umuhimu wa kuhifadhi mazao yao kwa pamoja na kuweza kupata mnunuzi hasa katika kipindi ambacho mazao yamekuwa ghali na hivyo kuweza kunufaika na kilimo.

Hata hivyo aliiomba Halmashauri hiyo kuweka utaratibu wa upatikanaji wa dawa ya kuulia panya waharibifu wa mazao pindi linapotokea baa badala ya kusubiri dawa kutoka Halmashauri kuu ambayo mara nyingi huchelewa na hivyo wakulima kuishia kupata hasara.

Awali mmoja wa waraghibishi kutoka TGNP- Mtandao Donald Kipondya alisema, mitazamo ya kisiasa inachangia kudhoofisha huduma za kijamii ikiwemo huduma za maji katika kijiji cha Bamba – Fulwe kata ya Mikese kufuatia uongozi wa kijiji kuwatangazia wananchi kuwa huduma za maji bure jambo ambalo si kweli.

Kipondya alisema, mradi huo mkubwa wa maji wenye thamani ya zaidi ya Sh. 2 bilioni unaohudumia wakazi kutoka katika vijiji viwili vya Bamba na Fulwe kwenye kata hiyo unaweza usiwe endelevu ikiwa wananchi hao hawataweza kuchangia.

Hata hivyo aliiomba Serikali kufirikia kwa makini kupeleka mradi wa maji kwenye kata ya Mngazi iliyopo wilayani humo ambayo wakazi wake wanatumia visima vitano vya maji ambavyo viwili tu hutoa maji baridi na vitatu maji ya chumvi huku wakitegemea zaidi maji ya mto na kufanya kuwa hatarini katika kupata magonjwa ya mlipuko ikiwemo kipindupindu.

Akizungumzia suala la Maji Injinia wa Maji wa wilaya hiyo Mhandisi Beatus Sanane alisema, Halmashauri imekuwa na utaratibu wa kuweka kipaumbele cha maji kwa eneo hilo kwenye bajeti lakini kwa sasa kitaweka msisitizo kwenye bajeti ya mwaka 2018/19 ili kufanya wananchi hao kupata maji ya uhakika.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo ambaye pia ni Afisa Nyuki, Fatma Mbukuzi aliiomba TGNP-Mtandao kusaidia katika kuelimisha jamii ikiwemo suala zima la umuhimu wa kuchangia maji kwani kwa sasa maji ni bidhaa na sio bure kama ilivyokuwa zamani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

Habari Mchanganyiko

Dk. Gwajima atoa maelekezo kwa maofisa maendeleo nchini

Spread the love  WAZIRI wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii Jinsia Watoto,...

Habari Mchanganyiko

Kairuki awaweka mtegoni wakurugenzi watakaoshindwa kufikia malengo ya makusanyo

Spread the loveWAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na...

error: Content is protected !!