May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uzito uliopitiliza janga jipya kwa vijana

Spread the love

 

UZITO wa mwili uliopitiliza umetajwa kuwa janga jipya kwa vijana, hasa wenye umri kati ya miaka 10 hadi 19. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Alhamisi, tarehe 12 Agosti 2021 na Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), nchini Tanzania, Dk. Mariam Ngaenje, katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana, yaliyofanyika jijini Dodoma.

Dk. Ngaenje amesema, vijana milioni 207 kati ya bilioni 1.2 (asilimia 17.3), duniani, wanakabiliwa na tatizo hilo, linalosababishwa na watu kutofuata mlo kamili.

Aidha, Dk. Nhgaenje amesema katika kundi hilo, wasichana wako katika hatari kubwa ya kupata tatizo la utapiamlo.

“Mbali na hayo, watoto wa kike wapo katika hatari zaidi ya kupata utapia mlo na athari za mila na desturi, ambazo zisababisha ukosekanaji wa vyakula vyenye virutubisho, elimu bora na fursa za Kiuchumi,” amesema Dk. Ngaeje.

Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la Idadi ya Watu (UNFPA), nchini Tanzania, Dk. Mariam Ngaenje

Ili kukabiliana na changamoto hizo, Dk.Ngaeje amesema UNFPA imedhamiria kusaidia vijana na taasisi zao, kupitia mkakati wa shirika hilo wa kusaidia vijana unaoitwa “My Body ,My life,My World”.

“Tumedhamiria kuwa, kila kijana atapata elimu, taarifa sahihi, huduma na anakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi juu ya mwili na maisha yake. Pia, anapata nafasi ya kushiriki katika mipango na utekelezaji wa programu za vijana ili kuleta mabadiliko katika jamii,”amesema Dk.Ngaenje.

 

Naye Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Patrobas Katambi, amesema Serikali imewekeza nguvu kubwa katika kuweka mikakati ya kuwawezesha vijana.

Katambi amesema, kupitia mikakati hiyo Serikali imeweka utaratibu wa kuwawezesha vijana kiuchumi, kijamii na kiafya.

error: Content is protected !!