May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Uzinduzi Royal Tour: Rais Samia atoa shukrani

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametoa shukrani kwa wote waliohusika katika maandalizi ya uzinduzi wa Filamu ya The Royal Tour nchini humo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha …(endelea).

Filamu hiyo baada ya kuzinduliwa maeneo mawili nchini Marekeani, jana Alhamisi tarehe 28 Aprili 2022 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk. Philip Mpango.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia leo Ijumaa ameandika, “nawashukuru wananchi wa Arusha, wadau wa utalii, uongozi wa mkoa, kamati ya Royal Tour na wote walioshiriki na kufanikisha uzinduzi wa 3 wa filamu ya Royal Tour jijini Arusha.”

“Nafarijika kuona mapokezi haya makubwa ya zawadi niliyowaandalia Watanzania. Kwa pamoja tutafanikiwa.”

Uzinduzi wan ne utafanyika tarehe 7 Mei 2022 Zanzibar na 8 Mei 2020 utakuwa jijini Dar es Salaam.

error: Content is protected !!