May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Madini yapokea fedha kiduchu za miradi ya maendeleo

Waziri wa Madini, Dotto Biteko

Spread the love

 

WIZARA ya Madini imepokea Sh 1.5 bilioni pekee kwaajili ya miradi ya maendeleo hadi kufikia Machi 2022 sawa na asilimia 10 ya Sh 15 bilioni zilizopangwa kwa mwaka wa fedha 2021/22. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yamebainishwa leo Ijumaa tarehe 29 Aprili, 2022 na Waziri wa Madini, Doto Biteko, wakati akiwasilisha hotuba ya makaditio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2022/23.

Biteko amesema hadi kufikia Machi, 2022, Wizara imepokea jumla ya shilingi bilioni 39.0 kutoka Wizara ya Fedha na Mipango na kati ya fedha hizo shilingi bilioni1.5 ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo na shilingi bilioni 37.5 kwa ajili ya matumizi ya kawaida.

Hata hivyo amesema katika Mwaka 2021/2022 Wizara ilitengewa bajeti ya shilingi bilioni 66.8 kwa ajili ya matumizi ya Wizara na taasisi zake.

“Kati ya fedha hizo, shilingi bilioni 15.0 zilitengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo na shilingi bilioni 51.8 kwa ajili ya matumizi ya kawaida,” amesema Biteko.

error: Content is protected !!