Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Uwanja wa ndege Chato, waibua mapya
Habari za SiasaTangulizi

Uwanja wa ndege Chato, waibua mapya

Uwanja wa Ndege wa Chato wakati unajengwa
Spread the love

SERIKALI imeamua kupandisha hadhi baadhi ya mapori ya akiba kuwa hifadhi za taifa yaliyopo kwenye mikoa ya Geita na Kigoma, ili kujisafisha na tuhuma za upendeleo katika ujenzi wa uwanja wa ndege wa Chato, mkoani Geita. Anaripoti Mwandishi Wetu kutoka Dodoma … (endelea).

Miongoni mwa mapori ambayo yamepandishwa kuwa hifadhi, ni pamoja na pori la akiba la Biharamulo, Burigi, Kimisi, Ibanda na Rumanyika – Orugundu, yaliyopo katika mikoa ya Geita na Kigoma. 

Tangu serikali ya Rais John Pombe Magufuli, ifanye uamuzi wa kujenga uwanja wa ndege wa Chato, kumeibuka malalamiko ya upendeleo kutoka kwa baadhi ya wananchi, hasa wachumi na wanasiasa wa upinzani.

Wanaopinga ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Chato, wanajiegemeza kwenye hoja kuwa, uamuzi ya serikali, tokea Awamu ya Kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere, iliamua kuwa Uwanja wa Kimataifa wa Mwanza, ndio uwanja mkuu wa kuunganisha nchi na mataifa mengine ya Maziwa Makuu.

Mpaka sasa, serikali ina hifadhi za taifa 16 na kwamba, kati ya hizo ni hifadhi tano pekee ambazo zinajiendesha kwa faida.

Kwa mujibu wa Sensa ya Taifa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012, Mji wa Chato una wakazi 17,508 (elfu kumi na saba, laki tano na nane elfu).

Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizobahatika kuwa na vivutio vingi vya utalii katika ukanda wa Afrika.

Kwa mujibu taarifa kutoka ndani ya serikali, Tanzania ina eneo la kilometa za mraba 945,234. Kati ya eneo hilo, takribani robo ya eneo hilo – Sq.km 236,308.8 – imeachwa kwa ajili ya matumizi ya wanyama pori.

Usimamizi wa maeneo ya wanyamapori unahusisha hifadhi za taifa 16 zinazosimamiwa na TANAPA, mapori ya akiba 28 na mapori tengefu 42 ambayo yanasimamiwa na TAWA.

Aidha, mapori ya Ibanda na Rumanyika yanazungukwa na Kata 12 zenye vijiji 24. Kwa ujumla ni kuwa eneo ambalo limepandishwa hadi lina jumla ya kata 30 na vijiji 72.

Hata hivyo, mapori ambayo yamepandishwa hadhi, yanakaliwa na wafugaji wengi; mara nyingi, maeneo haya yamekuwa na mgogoro baina yao na serikali katika kutafuta maeneo ya malisho ya mifugo yao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

Habari za Siasa

Mgongano wa kimasilahi wamhamisha Chande TTCL

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),...

Habari za SiasaTangulizi

Mgawo wa umeme: Rais Samia ampa miezi sita bosi mpya TANESCO

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amempa miezi sita Mkurugenzi...

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

error: Content is protected !!