Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Utafiti Twaweza: Uchumi tatizo kubwa linalosumbua kaya
Habari Mchanganyiko

Utafiti Twaweza: Uchumi tatizo kubwa linalosumbua kaya

Spread the love

 

MATOKEO ya utafiti uliofanywa na Taasisi ya TWAWEZA kati ya tarehe 18 Juni na 12 Julai 2022 kwa wahojiwa 3,000 waliopigiwa simu, yameonesha kuwa nusu ya wananchi wanataja kupanda kwa gharama za maisha na kukosa fursa za kuzalisha kipato. Anaripoti Felister Mwaipeta, TUDARCo …  (endelea).

Matokeo ya utafiti huo ambao muhktasari wake umewasilishwa leo tarehe 25 Agosti, 2022 na Mkurugenzi Mtendaji wa TWAWEZA, Aidan Eyakuze, yamebainisha kuwa matatizo makubwa matatu ambayo yalitajwa kuwasumbua zaidi wananchi kwenye kaya zao yote ni matatizo ya kiuchumi.

Kati ya hayo, tatizo kubwa zaidi ni kupanda kwa bei za bidhaa na gharama za maisha ambao ni sawa na asilimia 48, asilimia 29 ni ukosefu wa ajira na fursa nyingine za kuzalisha kipato, vile vile matatizo ya njaa na uhaba wa chakula yanatajwa na wananchi wengi sawa na 26.

Katika utafiti huo mbali na matatizo ya kiuchumi wananchi wametaja matatizo mengine kwenye huduma za jamii: vituo vya afya (23%), upatikanaji wa maji safi (20%), huduma za usafiri (17%) na mapungufu katika sekta ya elimu (15%).

Twaweza imetoa matokeo hayo kwenye jarida la utafiti lenye kichwa cha habari Hali ya Taifa – Uchumi: Uzoefu na maoni ya wananchi wa Tanzania kuhusu uchumi wa Taifa na tozo za miamala ya fedha kupitia simu.

Muhtasari huo unatokana na takwimu kutoka Sauti za Wananchi, utafiti wa kwanza barani Afrika wenye uwakilishi wa kitaifa unaofanyika mara kwa mara kwa njia ya simu za mkononi.

Takwimu zilizowasilishwa zilikusanywa kutoka jopo maalumu la wahojiwa wa tafiti za awali zilizofanywa na Ipsos nchini Tanzania.

Wahojiwa walichaguliwa kinasibu, na jopo lilikuwa na uwakilishi wa kitaifa. Takwimu hizi ni za awamu ya saba ya utafiti kwa njia ya simu, ambapo jopo la wahojiwa 3,000 walipigiwa simu kati ya tarehe 18 Juni na 12 Julai 2022.

Aidha, walipoulizwa ni jambo gani ambalo wangependa Rais kulishughulikia kama suala la kipaumbele, asilimia 46 ya wananchi walitaja kupanda kwa gharama za maisha na asilimia 42 hali ya vituo vya afya.

Eneo la tatu linalotajwa na wengi kama kipaumbele cha kushughulikiwa na Rais, asilimia 35 walitaja huduma za usafiri, asilimia 44 walitaka serikali zao za mitaa ziboreshe utoaji wa huduma za jamii, hasa huduma za usafiri, vituo vya afya na asilimia 26 walitaja upatikanaji wa maji safi kama vipaumbele vyao vikuu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!