August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Usiri thamani halisi ya ardhi yatajwa changamoto kwa wathamini

Spread the love

 

ASILIMIA kubwa ya migogoro ya ardhi kwa upande wa uthamini unasabishwa na wahusika kushindwa kutambulisha mali zao kwa usahihi. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Hayo yameelezwa leo tarehe 4 Agosti 2022, na Mthamini kutoka Ofisi ya Mthamini Mkuu Dodoma, Mwikari Mshana alipokuwa akizungumzia na waandishi wa habari katika banda la maonesho la wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwenye viwanja vya nane nane Nzuguni Jijini Dodoma.

Mshana amesema kuwa asilimia kubwa ya wamiliki wa ardhi na wanunuzi hawasemi ukweli juu ya uhalisia wa thamani halisi ya ardhi na inapofikia hatua ya uthamini huleta malalamiko.

Ameendelea kueleza kuwa hali hiyo husababisha malalamiko mengi kuelekezwa wizara ya ardhi kitengo cha uthamini wakati sababu kubwa ni wao kwa kushindwa kuwa wakweli juu ya mali wanazozimiliki na thamani yake halisi.

“Jambo lingine ambalo ni changamoto katika uthaminishaji wa thamani ya ardhi ni pale ambapo mmiliki halisi wa eneo kuchukua muda mrefu bila kuendeleza eneo na kupelekea majirani ambao wamemzunguka kumega ardhi na kusababisha kuwepo kwa migongano,” ameeleza Mshana.

Naye Msaidizi wa Kumbukumbu mabaraza ya Ardhi na nyumba Ramadhani Jingu ameeleza kuwa asilimia tisini ya watanzania waishio vijijini hawana elimu ya kutosha kuhusu matumizi bora ya ardhi.

Ameeleza kuwa kutokana na hali hiyo imekuwa ikisababisha migogoro mingi ya ardhi inasababishwa na jamii kutokuwa na elimu kuhusu matumizi bora ya ardhi.

Kutokana na hali hiyo amesema wizara imekuwa ikitoa elimu kwa wanachi kwa njia mbalimbali ili kuwaelimisha juu matumizi bora ya matumizi bora ya ardhi ili kuepukana na migogoro isiyokuwa ya lazima.

Hata hivyo ameeleza kuwa ni vyema kutoa elimu kuanzia ngazi ya sekondari pamoja na maafisa watendaji ili kueleza umuhimu wa matumizi ya ardhi.

error: Content is protected !!