Raia mmoja wa Korea Kusini amekamatwa nchini Urusi kwa madai ya ujasusi na kuzuiliwa katika mji wa mbali wa mashariki mwa nchi wa Vladivostok kabla ya kuhamishiwa Moscow kwa hatua za uchunguzi. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Shirika la habari la serikali ya Urusi – TASS jana Jumatatu limenukuu vyombo vya kisheria vikisema, mtu huyo amefahamika kwa jina la Park Won-soon.
Shirika hilo la habari la serikali limesema ni kesi ya kwanza dhidi ya raia wa Korea Kusini.
Wizara ya mambo ya nje ya Korea Kusini ilisema katika taarifa kwamba ubalozi wake mdogo ulimsaidia raia wake tangu ulipopata taarifa ya kukamatwa kwake.
Hata hivyo, ubalozi huo umejizuia kutoa maelezo zaidi kwa sababu suala hilo linaendelea kuchunguzwa.
Urusi inaichukulia Korea Kusini kama nchi isiyo rafiki kwa sababu ya uungaji mkono wa Seoul kwa vikwazo vya nchi za Magharibi dhidi ya Moscow juu ya vita vya Ukraine.
Leave a comment