Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Ununuzi korosho pasua kichwa, mbunge aiangukia Serikali
Habari Mchanganyiko

Ununuzi korosho pasua kichwa, mbunge aiangukia Serikali

Zao la Korosho
Spread the love

 

ABDALLAH Chikota, mbunge wa Nanyamba (CCM), mkoani Mtwara (CCM), ameiomba Serikali iweke bei elekezi ya zao la korosho katika mfumo wa soko la awali, ili kuondoa changamoto ya viwanda vya ndani kukosa malighafi ya zao hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Akizungumza bungeni jijini Dodoma, leo Jumatano tarehe 19 Mei 2021, Chikota amesema wakulima wa zao hilo wanagoma kupeleka korosho kwenye soko hilo, kwa kuwa bei yake haina maslahi.

“Kwa kuwa utaratibu huu wa mfumo wa soko la awali, huwa unakutanisha wenye viwanda na wakulima, lakini hauna ushindani sababu bei ni ndogo na wakulima hawavutiwi kupeleka korosho zao, kama ilivyo kwenye minada mingine ya kawaida,” amesema Chikota.

Chikota amehoji “Je, Serikali ina mpango gani kuweka ‘top up’ kwa bei ile waliyokuja nayo wawekezaji ili kuhakikisha wawekezaji hao wanapata korosho.”

William Ole Nasha, Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji

Chikota amesema, changamoto hiyo inasababisha viwanda vingi vya korosho kufanya kazi chini ya uwezo wake, kutokana na kukosa malighafi ya zao hilo kutoka kwa wakulima.

“Takribani viwanda vyote vinafanya kazi chini ya uwezo wake kutokana na changamoto mbalimbali, ikiwemo ukosekanaji wa malighafi sababu hawapati korosho mnadani. Serikali inatoa kauli gani kwa wawekezaji waliofungua viwanda nchini na wale wanaotarajia kufungua?” Amehoji Chikota.

Akijibu maswali hayo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, William Ole Nasha, amesema Serikali itaboresha mfumo huo ili kuwavutia wakulima kuuza korosho zao.

“Kuhusu swali kwamba kuna changamoto korosho kupatikana sababu wakulima hawana imani na mfumo wa soko la awali, nataka nimhakikishie mbunge kwamba, kwa kuwa mfumo umeanza serikali itachukua jitihada kuboresha ili kuweza kuvutia wakulima,” amesema Ole Nasha na kuongeza:

“Tutaboresha ili waone kuwa ile sio kangomba, bali soko lipo lenye lengo kuhakikisha viwanda vya ndani vinapata korosho kwanza kabla ya nje.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!