May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba: Ama zetu, Ama zao, mashabiki elfu 10 ruksa

Haji Manara, Msemaji wa Simba

Spread the love

 

KUELEKEA mchezo wa marudiano wa Ligi Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs, klabu ya Simba imekuja na kauli mbiu ya ‘Ama zetu, Ama zao’ ambayo yenye lengo la kupindua matokeo ili waweze kufuzu kwenye hatua ya nusu fainali. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Mchezo huo wa robo fainali utachezwa siku ya Jumamosi ya tarehe 22, Mei 2021 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, majira ya saa 10 jioni.

Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema kuwa timu hiyo itahakikisha inafuzu licha ya kuruhusu mabao 4-0, ugenini na wataingia na slogani ya ‘Ama zetu, Ama zao’.

“Wanasimba wanataka kufuzu, hatutaki kujitahidi, Simba siyo timu ya kujitahidi, ni timu ya kufuzu na mashabiki wanaamini timu yao inaweza na kauli mbiu yetu itakuwa Ama zeta ma zao,” alisema Haji.

Katika hatua nyingine msemaji huyo, amesema kuwa mpaka sasa wameruhusiwa kuingiza mashabiki 10,000 licha ya kufanya juhudi za kutaka kuongezewa.

“Mpaka sasa tumeruhusiwa mashabiki 10,000 lakini tunaendelea kuomba kuongeza, naomba uwanjani rangi iwe nyekundu na nyeupe,” aliongezea Haji.

Ili Simba ifuzu kwenye hatua ya nusu fainali inahitaji kupata ushindi wa bao 5 na kuendelea bila kuruhusu nyavu zao kuruhu bao.

Kikosi hiko kilirejea Jumatatu kutokea Afrika Kusini na siku ya jana Jumanne ya tarehe 18 Mei, 2021 waliingia kambini kwa kuanza maandalizi ya kuwawinda Kaizer Chiefs ambao watawasili muda wowote kuanzia leo.

error: Content is protected !!