Sunday , 28 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Ukitumia VPN faini mil. 5, kifungo mwaka 1
Habari MchanganyikoTangulizi

Ukitumia VPN faini mil. 5, kifungo mwaka 1

Spread the love

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imewataka wananchi kwa ujumla na kampuni ambazo kwa asili ya majukumu na kazi zao, matumizi ya mtandao binafsi (VPN) hayazuiliki, kutoa taarifa TCRA juu ya VPN wanazotumia.

Pia imewataka kutoa taarifa zote muhimu ikiwemo anuani ya itifaki ya mtandao kabla ya Oktoba 30, mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Katika taarifa iliyotolewa na TCRA kwa umma, leo Ijumaa imeeleza kuwa imebaini upatikanaji wa maudhui yaliyokatazwa kwa kupitia matumizi ya mtandao binafsi (VPN) kinyume cha kanuni.

“Kanuni ya 16(2) ya Kanuni za Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta kuhusu Maudhui Mtandaoni za mwaka 2020, mtu hatatoa, hatamiliki au hatasambaza teknolojia, programu, programu tumizi au kitu chochote kinachoendana na ambacho kinaruhusu au kumsaidia mtumiaji kupata maudhui yaliyokatazwa,” imeeleza taarifa.

Aidha, TCRA imesema itaendelea kuchukua hatua za kiudhibiti dhidi ya matumizi ya VPN yasiyo halali ikiwemo kuzuia upatikanaji wa VPN ambazo hazijatolewa taarifa au kusajiliwa na kuongeza kuwa, yeyote atakayebainika adhabu yake ni faini isiyopungua Sh 5 milioni au kifungo cha mwaka mmoja au vyote kwa pamoja.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mvungi aendesha kikao kazi cha wataalam wa Regrow

Spread the love  MKURUGENZI wa Idara Sera na Mipango Wizara ya Maliasili...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari Mchanganyiko

Polisi wakanusha kufanya uzembe ajali iliyouwa mwandishi Ayo Tv

Spread the loveJESHI la Polisi limekanusha tuhuma zilizoibuliwa dhidi yake  kwamba limekawia...

error: Content is protected !!