Saturday , 4 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Ukatili wa kijinsia: Wanaume walia kupigwa, kunyimwa unyumba
Habari Mchanganyiko

Ukatili wa kijinsia: Wanaume walia kupigwa, kunyimwa unyumba

Spread the love

 

IKIWA dunia inaadhimisha siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, wanaume wamefunguka kuhusu vitendo hivyo huku madai ya kunyimwa unyumba na vipigo yakitikisa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Madai hayo yameibuliwa Leo Jumamosi, tarehe 10 Desemba 2022, wakizungumza na MwanaHALISI Online, katika maadhimisho ya siku ya haki za binadamu duniani, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Mwanaume mmoja ambaye hakutaka kutaja jina, ameueleza mtandao huu kuwa, baadhi ya wanaume ikiwemo na yeye, huwa wanakabiliwa na ukatili wa kijinsia kutoka Kwa wake au wenza wao, ikiwa pamoja na kunyimwa haki ya ndoa (unyumba) na kupigwa bila sababu za msingi.

“Mimi nakueleza lakini sitaki kukutajia jina langu, Mimi binafsi ni mhanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia mke wangu ananipiga, wakati mwingine bila sababu ananinyima unyumba. Lakini haya mambo hatuyazungumzi Kwa sababu ya kuchekwa na jamii,” amesema mwanaume huyo ambaye hakutaka kutaja jina.

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), Kanda ya Magharibi, Alex Luwoga, amesema vitendo vya ukatili dhidi ya wanaume vinatokea katika jamii, lakini havisikiki kutokana na wahusika kufanya Siri wakiogopa kuchekwa na jamii.

Amesema zipo sababu nyingi zinazowafanya wanawake wawafanyie wanaume ukatili, ikiwemo Hali ya kiuchumi.

“Kwenye Kanda ya Magharibi tunapokea sana malalamiko hayo na kiuhalisi ni machache. Lakini wapo wanawake wanapiga waume zao, kina mwanamke mwenye uchumi mkubea kuliko mume anatumia kigezo hicho kama fimbo. Malalamiko mengine wanaume wanalia kunyimwa unyumba,” amesema Luwoga.

Mkurugenzi wa Shirika la Wanahabari la Kutetea Jamii za Pembezoni (MAIPAC), Mussa Juma amesema “ukatili ni mkubea, utakuta wanaume hawapendi kuzungumza wangepata platform ya kuzungumza ingekuwa janga. Mwanamke akiwa na uchumi mkubwa na uwezo wa kuendesha familia bila kutegemea mwanaume inakuwa tabu.”

“Wanawake wenye kazi zao wanaongoza kufanya ukatili wa kijinsia wanataka kuwa juu ya mume wako. Unakuta mwanaune analea familia peke take mama Yuko VICOBA na vikundi vingine pamoja na kazi badala ya kuangalia familia,” amesema Juma.

Juma amesema inahitajika mjadala wa kitaifa kujadili madhila wanayokumbana nayo wanaume kutoka Kwa wake na wenza wao, hususan za kupigwa na kunyimwa unyumba.

“Ukatili ndani ya familia upo mkubwa sana, wanaume wananyimwa unyumba hasa na wanawake wenye vipato vikubwa na wasomi. Anataka akiwa na hamu ndio anatoa haki ya ndoa wewe ukitaka hatoi. Usione wanaume wanakesha baa ukadhani wanapenda, wengine wanakwepa kurudi nyumbani mapema wakihofia vitendo vya ukatili,” amesema Juma.

Mzee Rajab Shaban, amesema Mila na desturi zinawafanya wanaume washindwe kuweka wazi ukatili wanaokutana nao “Mila za kiafrika kikwazi, mwanaumr ukisema unaligwa na mke wako watu hawakuamini. Siku hizi mwanamke akiwa na uwezo wa kifedha basi umekwisha.”

Kwa upande wake Edison Mwakyembe, kutoka Taasisi ya Rights for Social Change Organisation (RSCO), iliyoko Mbeya, amesema elimu inahitajika ili kuwapa uelewa wanaume juu ya umuhimu wa kuibua ukatili wanaofanyiwa ili vitokomezwe.

“Changamoto ziko nyingi sana, mfano kwetu Mbeya matukio ya wanawake kuwapiga wanaume na kuwafukuza yako mengi hususan katika miezi ya mavuno kuanzia Aprili na Mei, wanawake wanatumia wanaume kama nguvu kazi ya kilimo, wakivuna wanawafukuza. Wengine wanaachiwa watoto,” amesema Mwakyembe.

Irine Clemence, mtetezi wa haki za binadamu, amesema kweli Kuna baadhi ya wanawake wanatekeleza vitendo hivyo, huku akiitaka jamii iongeze maadili katika kulea watoto wa kike Ili kutokomeza ukatili dhidi ya wanaume.

“Ni kwweli madai hayo yapo, hata sisi katika shughuli zetu za utetezi wa haki za binadamu tunapokea malalamiko hayo. Kikubwa malezi na maadili yameyumba ndiyo maana mwanamke anapata uthubutu wa kunyanyasa wanaume zamani haikuwa hivyo,” amesema Urine.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!