Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Uhaba wa  maji pasua kichwa kwa serikali
Habari Mchanganyiko

Uhaba wa  maji pasua kichwa kwa serikali

Wananchi wakiwa kaitka sehemu yemye Uhaba wa maji
Spread the love

SERIKALI imesema imeifanya  tathmini ya miradi ya maji yote nchini na kwa sasa inawekewa mipango sahihi ya kutekelezwa ili wananchi waweze kupata huduma ya maji kama ilivyokusudiwa, anaandika Dany Tibason.

Kauli hiyo imetolewa leo  mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo alipokuwa akijibu maswali ya Mbunge wa Monduli Julius Laizer (Chadema).

Katika swali lake, Mbunge huyo alihoji ni lini serikali itatekeleza ahadi ya Rais aliyoitoa wakati wa kampeni za Uuchaguzi Mkuu 2015 kuhusu ukarabati wa Mabwawa matatu ili wananchi wa Esilalei waweze kupata maji kwa ajili ya mifugo yao.

Akijibu maswali hayo,  Jafo alisema serikali katika mwaka wa fedha 2016/17 imekamilisha usanifu kwa ajili ya ukarabati wa Mabwawa ya Joshoni na Olkuro ili kubaini kuwa Sh.Bilioni 1.45 zinahitajika kwa kazi hiyo.

Alisema mahitaji hayo yatazingatiwa katika mipango na bajeti kwa mwaka wa fedha 2018/2019.
Aidha alisema serikali inaendelea na utekelezaji wa miradi ya maji katika vijiji vya Lendikinya kata ya Sepeko ambao unatekelezwa kwa gharama ya Sh.Milioni 868.07.

“Kazi imefikia asilimia 35 na itakamilika mwezi Oktoba 2017 kwa kuzingatia mkataba na mwaka 2017/18 serikali imeidhinisha Sh.Milioni 639.5 kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji katika kijiji cha Nanja,”alisema Jafo.

Kadhalika, alisema lengo la kufanya tathmini hiyo ni kujua nini kilichokwamisha baadhi ya miradi ili serikali iweze kutatua.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!