Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mbunge Kessy alia na maji Ziwa Tanganyika
Habari Mchanganyiko

Mbunge Kessy alia na maji Ziwa Tanganyika

Ziwa Tanganyika
Spread the love

IMEELEZWA kuwa tatizo la kushuka kwa kina cha maji ya Ziwa Tanganyika limesababishwa na kubomoka kwa banio la maji kwenye mto Lukuga (DRC), anaandika Dany Tibason.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba alitoa kauli hiyo leo asubuhi bungeni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Nkasi Kaskazini (CCM), Ally Kessy.

Kessy amesema katika miaka ya 1960 kulikuwa na kingo katika mto huo na kwamba zilisaidia kuzuia kupungua maji katika ziwa hilo.

“Je, nchi za Burundi, Zambia, DRC Congo na Tanzania zimefikia wapi katika mpango wa kuweka kingo katika mto Lukunga ili ziwa Tanganyika lisiathirike kwa kupungua maji na kutishia viumbe hai katika ziwa hilo,” amehoji Mbunge huyo

Akijibu swali hilo, Makamba amesema tatizo hilo linafuatiliwa kwa karibu na serikali kupitia Wizara ya Maji na Umwagiliaji.

Amesema mto huo ndiyo pekee unaotoa maji kwenye ziwa Tanganyika upande wa DRC kupeleka mto Congo na hatimaye kwenye bahari ya Antlantiki.

“Aidha, DRC na Tanzania kwa pamoja zinamiliki asilimia 86 ya ziwa lote(DRC-45%, Tanzania 41%, Burundi 8% na Zambia 6% na kushuka huko kwa kina cha maji ya ziwa kumeathiri shughuli za kiuchumi na kijamii,” amesema.

Amesema athari hizo ni pamoja na meli kubwa kushindwa kutia nanga ili kupakia na kupakua mizigo na abiria kwenye bandari za ziwa ambazo ni bandari ya Kigoma na Kasanga, Bunjumbura, Kalemia, Uvira na Moba na kwa upande wa Tanzania chanzo cha maji kwa mji wa Kigoma kinaathirika.

Hata hivyo, amesema hatua mbalimbali zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na mwezi Machi, 2014 wakuu wa nchi za Tanzania na DRC waliagiza mawaziri wan chi zote mbili wanaoshughulikia masuala ya maji wakutane ili kujadili namna ya kutekeleza mradi wa ujenzi wa banio hilo.

“Mawaziri walikutana na baada ya vikao hivyo Tanzania na DRC zilisaini Hati ya makubaliano(MoU) Mei 2015 ambapo zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 65 zinahitajika kujenga banio lililobomoka,” amesema.

Aidha, amesema nchi za Burundi na Zambia ambazo ni wanachama wa Mamlaka ya ziwa Tanganyika(LTA) zimeshirikishwa kuhusu ujenzi wa banio hilo na zinaunga mkono juhudi hizo.

Amesema jitihada nyingine za kutafuta fedha zinaendelea kwa kuwasiliana na wadau wengine wa maendeleo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!