March 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Walemavu wapaza sauti zao

Jenister Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu

Spread the love

CHAMA cha Viziwi Tanzania (CHAVITA) kinatarajia kuanzisha mradi maalum utakaosaidia viziwi na watendaji wa serikali za mitaa kufanya ufuatiliaji wa matumizi ya mafungu ya fedha za walemavu kwa kutoa mafunzo katika mikoa mitatu Mwanza, Arusha na Morogoro, anaandika Jovina Patrick.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Msafiri Mhando, Mratibu wa Miradi CHAVITA, amesema kumekuwepo na mafanikio katika malengo yao ikiwamo kuimarisha taasisi hiyo kwa kuboresha sera, kanuni na kurekebisha katiba.

Amesema bado kuna changamoto nyingi zinazokwamisha walemavu hao ikiwamo serikali na jamii kwa ujumla kutotilia mkazo utumiaji wa lugha za alama katika utoaji wa elimu pamoja na taarifa ya habari.

Kwa hiyo amesema CHAVITA kwa kufadhiliwa na The Foundation for Civil Society (FCS) itaanza kuendesha mkakati wa kutoa mafunzo kwa watendaji wa serikali za mitaa katika mikoa hiyo mitatu ili kupunguza changamoto hizi kwa walemavu hao.

Mradi huu utatekelezwa kwa muda wa miezi sita na CHAVITA imetenga 80,000,000/= kwa ajili ya kuutekeleza.

error: Content is protected !!