Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Udanganyifu, magonjwa yasiyo ya kuambukiza tishio NHIF
Habari MchanganyikoTangulizi

Udanganyifu, magonjwa yasiyo ya kuambukiza tishio NHIF

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu
Spread the love

 

WIZARA ya Afya imeeleza chanzo cha kuelemewa kwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya(NHIF), ni kuongezeka kwa idadi kubwa ya wananchi wenye magonjwa yasiyo ya kuambukizwa ambayo gharama zake ni kubwa. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Imetaja sababu nyingine inayohatarisha uhai na uendelevu wa Mfuko huo kuwa ni vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya watoa huduma na wanachama wa mfuko, ambapo imesema vitendo hivyo vinalenga kujipatia manufaa kinyume na utaratibu.

Hayao yamelezwa leo Septemba Mosi, 2022 jijini hapa na Waziri wa Afya,Ummy Mwalimu, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ambapo hatua hiyo imekuja baada ya kuibuka kwa sintofahamu hivi karibuni kuhusu mfuko huo.

Akifafanua kuhusu kulegalega kwa mfuko huo Waziri Ummy amesema kuwa mnamo Agosti 29 mwaka huu wakati akifungua Mkutano wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika kuhusu Ugonjwa wa Kipindupindu jijini Dar es Salaam,aliweka msisitizo wa kuweka nguvu na jitihada katika kuzuia magonjwa badala ya kusubiri kutibu.

“Katika muktadha huo nilitoa angalizo kuwa hivi sasa nchini kwetu tunashudia ongezeko kubwa la magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo matibabu yake ni gharama kubwa na hivyo kama tutachelewa kuchukua hatua stahiki katika kudhibiti magonjwa hayo, basi kuna hatari pia kwa Mfuko wetu wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuelemewa na gharama za matibabu kutokana na kuongezeka kwa idadi ya wanufaika wenye magonjwa yasiyoambukizwa, hali inayoweza kuathiri uhai na uendelevu wa Mfuko,”amesema.

Amesema kuwa kulingana na takwimu zilizopo, gharama za magonjwa yasiyo ya kuambukizwa zimeongezeka kutoka Sh 35.65 bilioni mwaka 2016/17 hadi Sh 99.09 bilioni mwaka 2021/22.

Amesema gharama za kuhudumia wagonjwa wa saratani wanaopata tiba za mionzi na chemotherapia (chemotherapy services), kupitia mfuko ziliongezeka kutoka Sh9 bilioni mwaka 2015/16 hadi kufikia Sh22.5 bilioni mwaka 2021/22.

Amesema kwa upande wa huduma za matibabu ya figo kwa wanachama wanaopata huduma ya kuchuja damu (hemodialysis services), gharama ziliongezeka kutoka Sh9.5 bilioni mwaka 2015/16 kufikia Sh 35.44 bilioni mwaka 2021/22.
“Pia idadi ya wagonjwa hawa wa figo imeongezeka kutoka 280 mwaka 2014/15 hadi kufikia 2,099 mwaka 2021/22,” amesema.

Ambapo gharama za matibabu ya moyo kwa wanachama wa Mfuko wanaopata matibabu ya upasuaji wa moyo (minimal and invasive cardiac procedures), ziliongezeka kutoka Sh 0.5 bilioni mwaka 2015/16 hadi kufikia sh 4.33 bilioni mwaka 2021/22, huku gharama za vipimo vya CT scan na MRI zikiongezeka kutoka sh 5.43 bilioni mwaka 2015/16 hadi kufikia sh 10.87 bilioni mwaka 2021/22.

Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga

“Kwa muelekeo wa takwimu hizi, ni wazi kuwa kama hatutachukua hatua madhubuti kama nchi, kuna uwezekano wa Mfuko kwa siku za mbeleni kushindwa kutimiza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria.

“Hatua hizo zinaanzia katika ngazi ya mtu mmoja mmoja kwa kubadili mtindo wa maisha kwa kuzingatia aina za vyakula tunavyokula, kuepuka uvutaji wa sigara na kufanya mazoezi hata hivyo Serikali kuendelea kubuni mikakati ya kukinga magonjwa haya na pia kupambana nayo kadri yanavyojitokeza,”amesema.

Akizungumzia vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na baadhi ya watoa huduma ya Afya,Waziri Ummy alisema katika mwaka wa fedha 2021/22 jumla ya wataaluma 65 wamefikishwa katika mabaraza yao kutokana na kukiuka taratibu na miongozo ya taaluma za afya.

Kutokana na hayo Waziri Ummy ameielekeza NHIF kuimarisha mikakati yake ya kupambana na vitendo vya udanganyifu pamoja na kuimarisha matumizi ya Mifumo ya TEHAMA.

Pamoja na hayo ametaja changamoto nyingine iliyopo ni uwepo wa kundi kubwa la wananchi wanaojiunga na NHIF kwa hiari ambao, takribani asilimia 99 ni wagonjwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

error: Content is protected !!