WACHEZAJI wa kimataifa Tuisila Kisinda pamoja na nyota kutoka Burundi Saido Ntibanzokiza wameng’ara dakika za mwisho wakati wa kufungwa kwa dirisha la usajili wa Ligi Kuu Taanzania Bara kwa msimu wa 2022/23. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)
Usajili huo wa dirisha kubwa uliodumu katika kipindi cha miezi miwili ulifungwa rasmi jana tarehe 31 Agosti 2022, majira ya saa 5:59 usiku.
Muda mchache kabla dirisha hilo kufungwa, Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara walifanikiwa kuinasa kwa mara nyingine, Saini ya nyota wao wa zamani raia wa Kidemokrasia ya Congo, Tuisila Kisinda akitokea nchini Morocco kwenye klabu ya RS Berkane ambao ni mabingwa watetezi wa michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Ujio wa Kisinda ndani ya Yanga, unamfanya kuwa mchezaji wa 14 kati ya 12 wanaohitajika kwa mujibu wa kanuni, huku kitendawili kikubwa kikiwa wachezaji gani wataondolewa ndani ya kikosi hiiko ili kutimiza idadi kamili inayoyotakiwa.
Kwa upande wa klabu ya Geita Gold ambao nao wanakibarua msimu huu cha kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika, hawakuwa nyuma kwenye dakika hizo za mwisho za usajili na kufanikiwa kumtangaza aliyekuwa mchezaji wa zamani wa klabu ya Yanga, Saido Ntibanzokiza.
Taarifa rasmi iliyotolewa na klabu hiyo, imeeleza kuwa mchezaji huyo raia wa Burundi amefanikiwa kuingia mkataba wa mwaka mmoja ambapo atakwenda kuongeza nguvu kwenye safu ya ushambuliaji ya klabu hiyo.
Ligi hiyo ambayo kwa sasa imesimama, itarejea tena tarehe 5 mwaka huu, mara baada ya kupisha kalenda ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF), katika kutafuta tiketi ya kufuzu kwa faib]nali za michuano ya kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani.
Leave a comment