April 13, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Uchaguzi ACT-Wazalendo waacha mpasuko, Kigogo wake ang’oka

Spread the love

Yeremia Kulwa Maganja, aliyekuwa Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, amejivua uanachama wa chama hicho, kwa madai kwamba kimegubikwa na hila. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Maganja ametangaza uamuzi huo leo tarehe 1 Aprili 2020, wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam.

Akitangaza uamuzi huo, amesema kilichomuondoa katika chama hicho ni ukosefu wa demokrasia pamoja na nguvu ya ACT-Wazalendo, kushikiliwa na kundi la watu wachache.

“Tulipohamia tuliweka mambo muhimu katika katiba ili kukiweka chama na kukijenga kiwe taasisi imara, tenganifu na viongozi wake, tukaona ili tufanikiwe tuliamini katika uhuru wa maamuzi ya vikao vya chama, na kudhibiti hila, ghiliba, ulaghai na mashinikizo, tukiamini ni matumizi mabaya.

Tulitaka viongozi wenye maamuzi sahihi yanayofaa wao na kwa wengine. Tungefanya hili tungepata uungwaji wa chama nje ya chama. Kwa bahati mbaya adhma yetu hii haijaweza kutimia,” amedai Maganja.

Katika sababu yake nyingine, Maganja amedai kwamba, Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, anasukumwa na masilahi yake binafsi.

Maganja amedai “Uongozi umeendelea kuwa dhaifu unaotegemea mtu, na si wa kitaasisi, utashi binafsi wa kiuongozi imekuwa uamuzi wa chama. Mfano mzuri wa ukosefu wa utekelezaji wa adhma tuliojiwekea ni kile uchaguzi mkuu ndani ya chama uliofanyika. Haikuhitaji uchunguzi kujua viongozi waliotangazwa walichaguliwa kabla ya mkutano mkuu wa uchaguzi.”

Maganja amedai kuwa, chama hicho kimevurugwa kutokana na ujio wa Maalim Seif Shariff Hamad na wafuasi wake, kutoka Chama cha Wananchi (CUF).

Maganja amesema Maalim Seif na wafuasi wake, wanataka kuhodhi mamlaka na nguvu ya chama hicho kutoka Tanzania Bara.

https://youtu.be/D-hVg3Lovy4

“Wanataka mamlaka kamili ya Zanzibar, Maalim Seif na timu yake wanataka katika chama watakachokuwa, lazima wahakikishe kitovu cha maamuzi, rasilimali na ushawishi vinakuwa Zanzibar na si kwingineko,” amedai Maganja na kuongeza:

“Hawa hawakuwa wameshajifunza kutokana na walioyakuta huko nyuma. Maalim Seif na timu yake wana yao. Vitu hivi vimekua vikisemwa pembeni nachukua nafasi hii kuzungumza hiyo.”

Maganja amedai kuwa, sababu nyingine iliyomfanya ahame ACT-Wazalendo ni uchaguzi huo ulikuwa uhuru wa kuchagua na kugombea.

“Kiongozi unakuja unasema mgombea fulani huyu hatakiwi unampiga vita ili asichaguliwe, ni dhahiri uhuru wa kuchagua wa uchaguzi na utashi wa kugombea vilikosekaana katika uchaguzi wa ACT- Wazalendo,” amedai Maganja.

Maganja amesema kwa sasa yeye na wafuasi wake, wako katika majadiliano ya kuamua wahamie katika chama gani cha siasa.

“Sijastaafu siasa, nitaendelea na siasa. Baada ya hapa nitakua na siku kadhaa za mashauriano na wenzangu,  ili kujua tutakwenda wapi. Tutaondoma ACT na tutaendelea kufanya siasa,” ameweka wazi Maganja.

error: Content is protected !!