Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Michezo Tyson Fury amtwanga Dillian Whyte
MichezoNgumi

Tyson Fury amtwanga Dillian Whyte

Spread the love

BINGWA wa masumbwi, Tyson Fury alimemtandika kwa KO mbabe mwenzie Dillian Whyte katika raundi ya sita na kutwaa taji lake la uzito wa juu la WBC. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Fury alimdondosha Whyte kwa pigo la uppercut ikiwa imesalia sekunde moja kuingia katika raundi ya sita.

Alijitahidi kusimama, lakini aliduwazwa vibaya na mwamuzi akamaliza pambano hilo lililokuwa limehudhuriwa na watazamani 94,000 katika Uwanja wa Wembley nchini Uingereza.

Fury (33) ambaye hajapoteza pambano amehusishwa na pambano la undisputed la dunia dhidi ya mshindi wa mechi ya marudiano kati ya Anthony Joshua na Oleksandr Usyk.

Hata hivyo, mbabe huyo amesema anapendekeza kustaafu kufuatia ushindi huo.

“Nadhani ndiyo ilivyo, inaweza kuwa pazia la mwisho kwa Mfalme wa Gypsy, njia bora kabisa ya kuaga.” Fury aliiambia BT Sport.

Whyte alianza pambano hilo kwa njia ya kustaajabisha katika raundi ya kwanza, hatua ambayo ilionekana kumkera Fury hapo awali, kabla ya kurejea kwenye raundi ya pili.

Tyson ameshinda mapambano 32 kati ya 33 akiwa ametoka sare pambano moja.

“Nilimwambia mke wangu mpenzi kule Paris, ningestaafu baada ya pambano dhidi ya Deontay Wilder itakua hivyo na nilimaanisha.

“Lakini nilienda na nikapewa nafasi ya kupigana Wembley na nafikiri ilikuwa kwaajili ya mashabiki wangu kuja na kupambana hapa.

“Sasa nimemaliza kila kitu, napaswa kuheshimu maneno yangu….njia bora kabisa ya kuondoka!” aliongeza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!