August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Drogba abwagwa urais Ivory Coast

Didier Drogba

Spread the love

 

MFUMANIA nyavu wa zamani wa Chelsea na timu ya Taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba amebwagwa kwenye kinyang’anyiro cha urais wa Shirikisho la Soka nchini humo baada ya kushika nafasi ya tatu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Katika uchaguzi huo uliofanyika jana tarehe 23 Aprili, Drogba amepata kura 21, mshindi wa pili Sory Diabate amepata kura 50 wakati mshindi wa kwanza Yacine Diallo akipata kura 59.

Kwa matokeo hayo sasa ni rasmi Diabate Sory na Idriss Yacine wanaelekea kwenye hatua ya pili ya mchakato wa kumpata Rais wa shirikisho nchini humo.

Mwaka jana Drogba (44) alijaribu kutupa kete katika uchaguzi huo lakini akaenguliwa kwa kukosa uungwaji mkono wa vilabu na wadau wa soka nchini humo hali iliyomkosesha sifa ya kuwania nafasi hiyo.

error: Content is protected !!