April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TRA: Nusu mwaka tumekusanya 15.9 Tril

Spread the love

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imekusanya kiasi cha Sh. 15.9 Trilioni katika kipindi cha nusu mwaka wa 2018/19. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa tarehe 31 Julai 2019 na Richard Kayombo, Kaimu Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi TRA, Makao Makuu.

Taarifa hiyo imeeleza, TRA imefanikiwa kukusanya kiasi hicho kati ya lengo la ukusanyaji wa Sh. 18 Trilioni kuanzia tarehe 1 Julai 2018 hadi 30 Juni mwaka huu

Aidha, taarifa hiyo imesema katika kipindi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha wa 2018/19 (mwezi Machi hadi Juni 2019), TRA ilikusanya Sh. 1.1 Trilioni mwezi Aprili, 1.2 Trilioni (Mei), na 1.5 trilioni (Juni).

“Kwa namna ya kipekee kabisa TRA inawashukuru walipakodi na wananchi wote kwa ujumla kwa ushirikiano,” inaneleza taarifa ya Kayombo.

error: Content is protected !!