Thursday , 7 December 2023
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Kifo cha Mhandisi Lwajabe: Maswali bila majibu 
Makala & Uchambuzi

Kifo cha Mhandisi Lwajabe: Maswali bila majibu 

Mhandisi Leopold Lwajabe, Mkurugenzi Msaidizi wa Miradi wa Wizara ya Fedha na Mipango
Spread the love

JESHI la Polisi jana tarehe 31 Julai 2019, lilitoa ripoti yake fupi ya uchunguzi kuhusu kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Miradi ya Umoja wa Ulaya (EU), katika Wizara ya Fedha, Mhandisi Leopord Lwajabe, (56). Anaandika Mchambuzi Wetu…(endelea).

Taarifa hiyo ilibeba ujumbe kwamba kifo cha Mhandisi Lwajabe, kilitokana na yeye mwenyeye kujinyonga. Polisi walisema, mhandisi huyo alikusudia kutenda kosa hilo la jinai na kuwa aliandaa na kuacha ujumbe maalum. 

Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salam kwenye taarifa ya jeshi hilo amesema, tarehe 26 Julai 2019 saa 02 asubuhi, walipokea taarifa za kifo cha Mhandisi Lwajabe kutoka kwa Mohamed Said, Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgoza, Mkuranga. 

Alisema tarehe 25 Julai 2019 saa 12 asubuhi, Mhandisi Lwajabe alitoka nyumbani kwake kwenda ofisini, na kwamba alitoka ofisini na kwenda kusikojulikana hadi tarehe 26 Julai 2019 alipogundulika akiwa amejinyonga huko Mkuranga.

Na kwamba mwili wake ulikutwa ukiwa umening’inia kwenye mwembe akiwa amejinyonga, na baada ya ukaguzi wa simu yake, ilibainika kuwa amefuta kila kitu. 

Taarifa ya Mambosasa imeacha matundu, haijajibu baadhi ya maswali yanayoweza kukinaisha masikio ya wengi.

Mhandisi Lwajabe alipata na misukosuko kwa siku 10 mfululizo, yaani kuanzia 16 Julai 2019 mpaka 26 Julai 2019. Taarifa hizi walikuwa nazo?

Kabla ya kupatikana kwake, Mhandishi Lwabaje alikuwa wapi? Alikuwa na nani? Kwanini walitoweka? Ni matarajio ya wengi taarifa ya polisi ingebeba majibu hayo.

Lakini baada ya Mhandisi Lwabaje kuonekana je, polisi walichukua hatua gani? Walimuhoji kuhusu kupotea kwake? Walianza kutafuta taarifa za mtekaji?

Je, katika tukio la kwanza waligundua nini? waliihoji familia yake? Alikuwa na matukio ya ugomvi na wenzake? Alikuwa ana tabia gani? Majibu ya maswali hayo ni muhimu.

Pia, taarifa za wanafamilia kwa Jeshi la Polisi zilipewa kumbukumbu namba CD/RB/4122/2019 na CD/RB/4259/2019; na kwamba, miongoni mwa maelezo yaliyotolewa na wanafamilia kwa polisi ni namba za simu mbili za mkononi alizokuwa akitumia Mhandisi Lwajabe wakati wa uhai wake.

Kuna la kujiuliza; Polisi waligundua chochote kupitia simu za marehemu?

Zipo tarifa kwamba, siku ya mwisho alipotoweka, aliaga kwenda kuonana na mtu aliyempigia simu. Polisi ilijishughulisha kutaka kujua ni nani aliyewasiliana naye?

Je, mtu huyo alienda naye wapi? Hapa minara ya kurusha mawimbi – satelaiti- inahusika; na mitambo ya swichi, ambazo ni kompyuta kubwa zenye uwezo wa kutunza tarifa ikiwemo namba ya mpiga simu, mpigiwa simu na tarifa zingine muhimu.

Bila shaka Jeshi la Polisi linao wataalam wenye weledi na mamlaka ya kukusanya tarifa za mawasiliano ya simu na kuzifanyia uchambuzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Tunastawisha ufisadi na kuchukia matunda yake

Spread the loveBUNGE la Jamhuri linaloendelea mjini Dodoma, kwa wiki nzima limetawaliwa...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Wamesahau aliyofanya Magufuli

Spread the loveJUMATATU ya tarehe 16 Oktoba 2023 itabaki kuwa siku ya...

error: Content is protected !!